AYA YA WIKI (JUMA LA 78)

ISHI NA MUONGOZO NA MAELEKEZO YA QUR-ANI, UFANIKIWE DUNIANI NA AKHERA. Unasubiri nini kuingia kwenye kundi la Waumini, wahi ufaidike kabla hujachelewa: “Enyi mlio amini! Rukuuni na msujudu, na muabuduni…

HADITHI YA WIKI (JUMA LA 78)

“Atakaye tawadha, akaeneza udhu (viungo vyote), kisha akaiendea swala ya faradhi, akaiswali pamoja na watu au pamoja na jamaa, au msikitini, Allah atamsamehe madhambi yake”. Muslim [232] na Ahmad [01/67]-Allah…

KATAZO LA WIKI (JUMA LA 78)

Kwa nini lakini unamfanyia husda na kumchukia mwenzako kwa sababu tu ya neema ya mali aliyo nayo?! Kwani wewe hutambui kwamba hiyo ni mipango yake Allah kumpa huyu zaidi, yule…

SWALI LA WIKI (JUMA LA 78)

SWALI: Ni jambo lililo tangaa na limekuwa kama ada katika jamii zetu, mwanamume kunyonya chuchu/maziwa ya mke wake. Naomba kufahamishwa hukumu ya sharia katika jambo hilo. JIBU: Mume kunyonya chuchu…

SOMO LA TANO – MUHAMMAD; MTUME WA MWISHO-Rehema na Amani zimshukie-Na uhusiano/mafungamano ya ujumbe (Da’awa) wake na jumbe za mbinguni zilizo tangulia.

“SIRA YA MTUME WA ALLAH; FALSAFA NA MAFUNDISHO YAKE” Mpendwa msomaji wetu-Allah akurehemu-kwa auni na uwezeshi wake Mola, tumekutana tena juma hili katika darsa zetu za Sira yake Bwana Mtume,…

YALIYO KARAHA KATIKA UDHU

1. Ni karaha kwa mwenye kutawadha kuacha suna yeyote miongoni mwa suna tulizozitaja chini ya anuani :SUNNA ZA UDHU.  Kwa sababu kuacha kuzitekeleza suna hizo kutampelekea mtu huyo kukosa thawabu,…

AYA YA WIKI (JUMA LA 77)

Ishi na muongozo na maelekezo ya Qur-ani, ufanikiwe duniani na akhera. Unasubiri nini kuingia kwenye kundi la Waumini, wahi ufaidike kabla hujachelewa: “Hakika Allah huwakinga walio amini. Hakika Allah hampendi…

HADITHI YA WIKI (JUMA LA 77)

“Atakaye tawadha kikamilifu, kisha akaswali rakaa mbili (Sunnatul-Wudhuu), akielekea (kwazo) kwa moyo wake na uso wake, imemuwajibikia pepo”. Nasaai [151], Muslim [234], Abu Daawoud [169] na Ahmad [04/158]-Allah awarehemu.

KATAZO LA WIKI (JUMA LA 77)

Hivi wewe unafikiri ni nani?! Mpaka lini utaendelea kuwadhulumu na kuwanyanyasa watu, eti tu kwa sababu ya madaraka yako, cheo chako, mali yako au nguvu zako?! Kumbuka madaraka yana mwisho…

SWALI LA WIKI (JUMA LA 77)

SWALI: Je, mke anafaa kumrithi mume aliye fariki muda mfupi tu baada ya ndoa? JIBU: Mke kumrithi mume wake ni jambo lililo thibiti kwa nassi (nukuu) ya Qur-ani. Angalia, marehemu…