MAANA YA TWAHARA KATIKA LUGHA YA SHERIA
“Twahara” ni neno la Kiarabu lenye maana mbili; maana ya kilugha na maana ya kisheria. “Twahara” katika lugha ina maana ya unadhifu na kujilinda na kila kilicho kichafu.
Kwa mtazamo wa sheria twahara ni kuondosha 1. Hadathi na 2. Kuondosha najisi.
- Hadathi ni hali inayomzuilia mtu kufanya ibada kama vile swala na hali hii huondoka kwa kutawadha ikiwa hadathi ni ndogo, na kwa kuoga ikiwa hadathi ni kubwa.
- Najisi ni kama vile damu, usaha, matapishi, choo kikubwa na kidogo, mbwa, nguruwe na kadhalika.