SWALA YA MSAFIRI

UTANGULIZI:

Allah Mola Mwenyezi anasema ndani ya Qur-ani Tukufu (muongozo sahihi wa wanadamu)

“….WALA HAKUWEKA JUU YENU MAMBO MAZITO KATIKA DINI….” (22:78)

Maana sahali ya kauli hii tukufu ya Allah ni kwamba waislamu hawakuwekea katika dini hii hukumu zisizotekelezeka kutokana na ugumu wake.

Bali hukumu zote za sheria ya Kiislamu zimezingatia maumbile na mazingira ya mwanadamu ili kumuwepesishia utekelezaji wake.

Uislamu unaizingatia safari kuwa ni kipande cha adhabu ambacho kinamkosesha mtu utulivu wake wa kawaida na kumyima mapumziko yanayohitajika na mwili wake.

Mtizamo huu wa Uislamu umeizingatia nafsi ya safari bila ya kuangalia chombo kinachotumika kusafiria.

Bali kiislamu safari ni safari tu hata kama ikiwa ni kwa ndege chombo ambacho kina uchovu kidogo tu, ukilinganisha na vyombo vingine vya usafiri.

Pia Uislamu haukuzingatia lengo la safari, safari yo yote itapewa hukumu ya safari muda wa kuwa si safari ya maasia na imefikisha umbali unaozingatiwa na sheria.

Kwa mtizamo huu juu ya safari ndipo Allah akamkhafifishia msafiri nyingi miongoni mwa hukumu za dini yake. Katika jumla ya hukumu hizo alizokhafifishiwa na swala.

Sasa kwa msaada wake Allah na tuanze kubainisha kaifia ya takhfifu hii sambamba na sharti zake na jinsi msafiri anavyofaidika nayo. Tuanze kwa kujiuliza:

1. SAFARI NI NINI?

Kisheria safari ni zile harakati/kitendo cha mtu kugura (kuhama/kuondoka) katika makazi yake ya asili kwenda mahala pengine ambapo umbali wake ni zaidi ya kilometa themanini na moja au maili khamsini (81km.150m) takriban.

Tunakusudia kwa neno letu (makazi ya asili) mahala ambapo alipozaliwa mtu na akakusudia/akaamua kuishi hapo. Hii ndiyo safari tunayoikusudia katika darsa yetu hii.

SWALA YA MSAFIRI

UTANGULIZI:

Allah Mola Mwenyezi anasema ndani ya Qur-ani Tukufu (muongozo sahihi wa wanadamu)

“….WALA HAKUWEKA JUU YENU MAMBO MAZITO KATIKA DINI….” (22:78)

Maana sahali ya kauli hii tukufu ya Allah ni kwamba waislamu hawakuwekea katika dini hii hukumu zisizotekelezeka kutokana na ugumu wake.

Bali hukumu zote za sheria ya Kiislamu zimezingatia maumbile na mazingira ya mwanadamu ili kumuwepesishia utekelezaji wake.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *