SWALI: Je, mke anafaa kumrithi mume aliye fariki muda mfupi tu baada ya ndoa?
JIBU: Mke kumrithi mume wake ni jambo lililo thibiti kwa nassi (nukuu) ya Qur-ani. Angalia, marehemu akiwa hana mtoto aliye zaa na mke huyo au mke mwingine, mjane wake atarithi robo ya mali yake. Na akiwa ameacha mtoto, mke atarithi thumni (1/8) ya mali ya marehemu mume wake. Hivyo ndivyo anavyosema Allah katika kauli yake: “…Na wake zenu watapata robo ya mlicho kiacha, ikiwa hamna mtoto. Mkiwa mna mtoto basi sehemu (fungu) yao ni thumni ya mlicho kiacha, baada ya wasia mlio usia au deni…”. An-nisaa [04]:12
Na hilo la mke kumrithi mume halikuwekewa sharti la kuishi nae muda mrefu au mfupi wala kuzaa au kutozaa nae, bali linathibiti kwa kufungwa kwa ndoa sahihi na si vinginevyo.
Allah ndiye Mjuzi mno.