SHARTI ZA MAAMUMA

Maamuma anayeswali nyuma ya imamu kumeshurutizwa sharti kadhaa ili kumfuata kwake imamu kusihi. Miongoni mwa sharti muhimu ni kama zifuatavyo:-

1)     Mfuataji (maamuma) asijue kubatilika kwa swala ya imamu wake au kuitakidi hivyo.

Mfano: Watu wawili wamefanya jitihadi katika kujua upande kilipo Qiblah.

Kila mmoja wa wawili hawa akaitakidi kwamba Qiblah kiko upande ule auonao yeye na wala hakiko upande auonao mwenzake.

Katika hali kama hii hakujuzu kwa mmojawapo wa wawili hawa waliokhitalifiana katika upande kilioko Qiblah, jambo ambalo ni mojawapo ya nguzo za swala.

Hakumjuzii kumfuata mwenzake  akamfanya kuwa ndio imamu wake na yeye akawa maamuma nyuma yake.

Kutokujuzu huku kunatokana na ile itikadi ya kila mmoja wa wawili hawa kwamba mwenzake amekosea welekea/upande wa Qiblah. Sasa basi, maadam amekosea Qiblah basi na swala yake anayoiswali kuelekea upande huo itakuwa sio sahihi, ni batili tu na si vinginevyo kwa itikadi yake hiyo.

2)    Imamu asiwe umiyi (asiyejua kusoma wala kuandika) na ilhali maamuma ni msomi:

Muradi wa makusudio ya “umiyi”, hapa ni mtu asiyeweza kuisoma vizuri Suratil-faatihah (Al-hamdu) kwa hukumu zake za usomaji kama zilivyotajwa katika vitabu vya fani ya “Tajweed”. Angalia ikiwa imamu na maamuma wote ni maumiyi, basi kutamjuzia kila mmoja wao kumfuata mwenzake.

3)    Imamu asiwe mwanamke na maamuma akawa ni mwanamume:

Mwanamke hana mamlaka kisheria kumtangulia mwanamume katika swala, akawa ndio imamu  wa mwanamume. Hili ndilo agizo la Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-katika kauli yake: “Mwanamke asimswalishe mwanamume”. Ibn Maajah-Allah amrehemu.

SHARTI ZA MAAMUMA

Maamuma anayeswali nyuma ya imamu kumeshurutizwa sharti kadhaa ili kumfuata kwake imamu kusihi. Miongoni mwa sharti muhimu ni kama zifuatavyo:-

1)     Mfuataji (maamuma) asijue kubatilika kwa swala ya imamu wake au kuitakidi hivyo.

Mfano: Watu wawili wamefanya jitihadi katika kujua upande kilipo Qiblah.

Kila mmoja wa wawili hawa akaitakidi kwamba Qiblah kiko upande ule auonao yeye na wala hakiko upande auonao mwenzake.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *