MTUME AANZA KUKUTANA NA MAKABILA

Baada ya safari ya Twaif, Bwana  Mtume – Rehema na Amani zimshukie – alirejea Makkah na kuuwahi msimu wa Hijja.

Makabila mbalimbali ya waarabu kutoka pande mbalimbali huja Makkah katika msimu huu kutekeleza ibada ya hijja na kutekeleza nadhiri zao kwa miungu masanamu sambamba na dhabihu zao (sadaka za kutekeleza)

Ilikuwa ni ada ya waarabu wanapofika  Makkah katika msimu huu wa hijjah, kuitumia vema fursa ya miezi mitukufu ya Hijjah kwa kufanya  biashara katika masoko ya Makkah. Masoko  mashuhuri yalikuwa ni matatu, ambayo ni ukaadhwi, Majannah na Dhul – Majaaz.

Waarabu walikuwa wakianza na soko la  ukaadhwi katika mwezi wa Dhul-qa’adah (mfunguo pili) wakikaa hapo siku kumi.

Kisha huelekea katika soko la Majannah ambako pia hufanya biashara kwa siku kumi. Halafu wakiuona mwezi muandamo wa Dhul-hijjah (mfunguo tatu) hao hushika njia na kuelekea katika soko la Dhul-Majaaz na soko  hili ndilo lililokuwa karibu zaidi na Makkah.

 Hufanya biashara hapo kwa siku nane tu, kisha  huelekea arafu kutekeleza ibada ya Hijjah.

Baada ya kupita muongo mmoja wa da’awah, yaani ile miaka kumi ambamo Bwana Mtume alikuwa akiwalingania jamaa zake uislamu kwa njia ya  upole na ulaini.

Aliazimia sasa kubadili mtindo/mbinu ya da’awah, kwa kuzielekeza nguvu zake katika masoko  haya  ya msimu ambako huko angekutana na watu kutoka sehemu mbalimbali na kuwafikishia  ujumbe wa Allah.

Makurayshi baada ya kuijua azma hii ya Mtume, wakapanga njama za pamoja ili kuitia doa da’awah hii na hatimaye kuibomoa kabisa, mbele ya kadamnasi ya makabila haya.

Mwanasira mkubwa; Ibn Is-haaq – Allah amrehemu – anaelezea katika kulisimulia hili –

“kwamba kundi la makurayshi lilimkusanyikia Al – waleed Ibn Al – Mughiyrah, huyu alikuwa ni mtu mzima wao nae alikuwa amefika kwenye msimu.

Akawaambia enyi Makurayshi, msimu ndio ushafika tayari na ujumbe (makundi) wa waarabu  utakujieni.

Watu hawa wameshalisikia  suala la  ndugu yenu huyu (Muhammad na dini yake). Sasa kongamaneni kwa rai moja tu (juu ya hili) na wala msitofautiane ikawa hawa wanakadhibisha wale na  kujibizana wenyewe kwa wenyewe.

Wakasema; Ewe Baba Abdi Shamshi sema wewe, tuambie wewe tuseme nini. Akawajibu; semeni nyinyi, mimi nitakusikilizeni wakasema; basi tuseme yeye kuhani.

Akawaambia; Wallah! Hapana yeye  si kuhani.

Tumewaona Makuhani hawako kama yeye. Wakasema; basi tuseme ni mwendawazimu. Akawaambia; yeye si mwendawazimu, tumekwishauo na kuujua  wazimu, yeye hana wazimu. Wakasema basi tuseme ni mshairi.

Akawaambia; yeye si mshairi, sisi tunaujua ushairi na fani zake zote, maneno ayasemayo si ushairi hata kidogo.

Wakasema; basi tuseme  ni mchawi. Akawaambia; Wallah ! kwa hakika maneno yake ni matamu sana  yenye kuvutia.

Hamtosema lolote kati ya yote haya mliyoyataja ila itajulikana kuwa ni uongo. Kauli ya karibu zaidi semeni; yeye ni mchawi, ameleta maneno ambayo yenyewe ni uchawi, humtenganisha kwa maneno hayo mtu na mwanawe, na baina ya mtu na mkewe na baina ya mtu na ndugu zake! wakatawanyika na kauli hii, wakawa wanawangojea watu majiani wanapokuja msimuni, hawapitii mtu yeyote ila humtahadharisha juu ya Mtume na kumuelezea khabari zake”.

Tusome na  tuwaidhike tukitaka;

(BASI NDIVYO HIVI HIVI, HAKUNA MTUME YEYOTE ALIYEWAJIA WALE WA KABLA YAO (hawa Makurayshi) ILA WALISEMA; “HUYU NI MCHAWI AU MWENDAWAZIMU” JE! WAMEUSIANA KWA (jambo) HILI? (La, hawakuusiana chochote) LAKINI (wote) WAO NI WATU WAOVU) (51: 52 – 53)

Makurayshi wakawa wanamfuata Bwana Mtume Rehema na Amani zimshukie – kila alipokwenda kila alipoliendea kabila miongoni mwa makabila yaliyofika msimuni kulifikishia ujumbe wa Allah, huja Mkurayshi mmoja akasimama mbele yake na kuwatahadharisha dhidi ya uchawi na vitimbi (hila) za Muhammad, kama walivyoona wao.

Mara nyingine wakimtuhumu kuwa ana wazimu, wakati mwingine wakisema ni muongo mzandiki na pengine huibuka na kusema, kuwa ni mchawi kwa kuwa Makurayshi walikuwa na hadhi na wakikubalika mbele ya waarabu wote, maneno yao haya yalipokewa kwa uzito mkubwa na wageni wao hawa na kuathiri kwa kiasi kikubwa kazi ya Mtume.

Miongoni mwa athari zilizoletwa na uzushi huu wa Makurayshi ni watu kumpuuza Mtume na alichokisema na kukataa kuitikia haki iliyo wazi.

Lakini yote haya, hayakumzuia Bwana Mtume kuendelea kuyafuata makabila na kuyafikishia ujumbe bila kujali upinzani wa Makurayshi.

Mtume alifanya hivyo huku akiamini kuwa haki itashinda tu hata kama itachukua muda mrefu na kwamba nusra ipamoja na subira, faraja imo ndani ya shida/matatizo na wepesi umo ndani ya uzito.

Msimu huu ukapita bila ya mafanikio yoyote Msimu uliofuatia, lilifika Makkah kundi la kabila la Khazraji.

Kundi hili likamsikia Mtume akiufikisha ujumbe kwa makabila, wakaziona alama na dalili za ukweli katika yale aliyokuwa akiyasema. Wakaambizana;

“Wallah! Huyu ndiye Mtume ambaye Mayahudi walikuwa wakikutisheni nae, basi wasikutangulieni kumuamini”.

 Mtume alipowafikishia ujumbe tu, mara moja wakamuamini na kumsadiki na wakataraji kuwa Mwenyezi Mungu ataleta suluhu baina yao kwa sababu ya Mtume huyu, wakamwambia Mtume;

“Hakika sisi tumeiacha kaumu yetu, hakuna kaumu yenye uadui na shari baina yao kuliko kaumu yetu, huenda, Mwenyezi Mungu akawaunganisha kwa ajili yako.

Tutawaendea na kuwafikishia ujumbe wako na kuwaelezea juu ya dini hii tuliyoifuata. Ikiwa Mwenyezi Mungu atakukusanyia watu hawa, basi hapatakuwa na mtu mtukufu kuliko wewe. Wakaagana na Mtume kukutana nae msimu wa mwaka ujao.

Kisha wakaondoka kurudi kwao Madinah wakiwa wamemsadiki na kumuamini Mtume. Walipofika kwao Madinah, walieleza jamaa zao habari za Mtume na kuwalingania Uislamu mpaka habari hizi zikaenea mji wote wa Madinah.

Hapakuwa na nyumba yoyote ya Maanswaari ila Mtume alitajwa humo. Huu ndio mwanzo wa kuingia Uislamu Madinah wakati huo mji ulikuwa ukiitwa “Yathribu” Darsa/somo hili halitakamilika ikiwa hatukuwataja na  kuwakumbuka vema  watu hawa na  mwanzo kutoka

Yathribu walioupokea kwa mikono miwili ujumbe wa Mtume wakamuamini na kuwa mabalozi wema wa Uislamu huko kwao Yathribu “Madinah”.  Kumbukumbu za kihistoria zinaonyesha kuwa watu hawa walipata sita na wote ni wa kabila la Khazraji. Watu hao ni:-

       1.As’ad Ibn Zaraarah, na

       2.Auf Ibn Al- Haarith. Wote hawa ni wa ukoo wa Najjar.

       3.Raafii Ibn Maalik wa ukoo wa Zariyq

       4.Qutwbah Ibn Aamir wa ukoo wa Salamah.

       5.Uqbah Ibn Aamir wa ukoo wa Hiraam na

       6.Jaabir Ibn Abdillah wa ukoo wa Ubayd Ibn Adiyyi – Allah awawiye radhi wote

 

MTUME AANZA KUKUTANA NA MAKABILA

Baada ya safari ya Twaif, Bwana  Mtume – Rehema na Amani zimshukie – alirejea Makkah na kuuwahi msimu wa Hijja.

Makabila mbalimbali ya waarabu kutoka pande mbalimbali huja Makkah katika msimu huu kutekeleza ibada ya hijja na kutekeleza nadhiri zao kwa miungu masanamu sambamba na dhabihu zao (sadaka za kutekeleza)

Ilikuwa ni ada ya waarabu wanapofika  Makkah katika msimu huu wa hijjah, kuitumia vema fursa ya miezi mitukufu ya Hijjah kwa kufanya  biashara katika masoko ya Makkah. Masoko  mashuhuri yalikuwa ni matatu, ambayo ni ukaadhwi, Majannah na Dhul – Majaaz.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *