DALILI YA SWALA NA TAREHE YAKE

Umethibiti ufaradhifu wa swala kwa kila muislamu ndani ya Qur-ani Tukufu, sunnah na Ijmaa.

Ama Qur-ani imeamrisha utekelezaji na swala katika makumi ya aya zake, miongoni mwake ni kauli tukufu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

”WALA HAWAKUAMRISHWA ILA KUMUABUDU ALLAH KWA KUMTAKASIA DINI (kwa ikhlaasi) WAACHE KUTOA ZAKKAH, HIYO NDIYO DINI ILIYO SAWA (98:5) Tuendelee kusoma.
“BASI MTUKUZENI ALLAH MNAPOINGIA KATIKA NYAKATI ZA USIKU (kwa kuswali Magharibi na Isha) NA MNAPOINGIA KATIKA ASUBUHI (kwa kuswali swala ya Alfajiri) NA SIFA ZOTE NJEMA NI ZAKE MBINGUNI NA ARDHINI NA (mtukuzeni) WAKATI WA ALASIRI NA MNAPOINGIA KATIKA WAKATI WA ADHUHURI” (30: 17-18)

Maelezo yaliyo katika mabano ni ufafanuzi wa aya kama ulivyo katika kauli ya swahaba Ibri Abaan – Allah amuwiye radhi. Tusome tena.
“KWA HAKIKA SWALA KWA WAUMINI NI FARDHI ILIYOWEKEWA NYAKATI MAKHUSUSI” (4: 103)

Ama katika sunnah, miongoni mwa hadithi za Mtume ambazo zimefunulia wazi kabisa kwamba swala ni nguzo miongoni mwa nguzo za Uislamu ni hizi zifuatazo:-

 

1. Imepokelewa hadhithi kutoka kwa Abdillah Ibn Umar-Allah awaridhe – kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu –Rehema na Amani zimshukie – amesema,

“Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano: Kushuhudia kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah na Muhammad ni Mjumbe wake (Shahada), na kusimamisha swala, kutoa Zakkah, kufunga Ramadhani na kuhiji kwa mwenye uwezo” Bukhaariy na Muslim.

 

2. Imepokelewa na Ibn Abbaas – Allah awaridhie kwamba Mtume – Rehema na Amani zimshukie – alimtuma Mua’adh – Allah amridhie – kwenda katika nchi ya Yemen (kulingania dini) akamwamiba

 “Walinganie (Waite) kutamka shahada kwamba hapana afaaye kuabudiwa kwa haki ila Allah na kwamba mimi Muhammad ni Mjumbe wa Allah, ikiwa wao watalitii hilo (watalikubali) basi wafahamishe kwamba Allah amefaradhisha juu yao swala tano mchana na usiku…………” Bukhaariy na Muslim.

 

3. Kauli yake Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie – alipomwambia yule mkazi wa majangwani ambaye alimuliza swala zilizo faridhi juu yake.

 “ Swala tano kila mchana na usiku” Yule mkazi wa majangwani akamuuliza (tena). Je, ninawiwa (ninalazimika) na swala nyingine zisizo hizo (tano) (Mtume) akamjibu “Hapana ila swala za suna” Bukhaary na Muslim.

 

Ama katika Ijmaa, wanazuoni wa Kiislamu wamekongamana na kuwafikiana bila ya khitilafu yoyote kwamba swala ni mojawapo ya nguzo za Uislamu.

Pia wamekongana kwamba yeyote mwenye kuiacha swala ama kwa kuifanyia mzaha au kwa kupinga anakuwa amejitoa mwenywe katika Uislamu.

Ama yule atakayeiacha kwa uvivu tu huku akikiri kuwa ni fardhi iliyomlazimu, huyu atakuwa na hatia na dhambi na atastahiki kupata adhabu ya hatia hiyo hapa hapo duniani na kule akhera.

Isitoshe kuwa ni karipio na onyo lenye kuupasuapasua moyo na mwenye kuacha swala kauli hii ya Mwenyezi Mungu Mtukufu 

 “NI KIPI KILICHOKUPELEKENI MOTONI? WASEME “HATUKUWA MIONGONI MWA WALIOKUWA WAKISWALI”.  (74:42-43).

Tunaambiwa katika aya hii kwamba siku ya kiyama Malaika watawauliza watu wa motoni.

Ni kipi/jambo gani lililokufanyeni nyinyi kuwa katika mafikio na marejeo haya mabaya motoni?

Hapo ndipo watu wabaya hawa, watu wa motoni watajibu kwa masikitiko na majuto makubwa, klichotufiksha mahala hapa pabaya ni kutoihifadhi kwetu ibada ya swala duniani (hatukuwa tukiswali).

Tukiangalia na kuipekuwa tarehe ya swala tutatambua kwamba swala ni ibada kongwe kabisa kufaradhishwa kwa wanadamu Mwenyezi Mungu Mtukufu anatusimulia khabari za Mtume Ismail – Amani imshukie

“ NA ALIKUWA AKIWAAMRISHA WATU WAKE SWALA NA ZAKA NA ALIKUWA MRIDHIWA MBELE YA MOLA WAKE”.(19:55)

Mwenyezi Mungu anazidi kutonyesha ukongwe na ibada hii ya swala kupitia ulimi na Nabii Issa – Amani imshukie

”……….NA AMENIUSIA SWALA NA ZAKA MAADAMU NI HAI” (19:31).

Mtume Muhammad – Rehema na Amani zimshukie – alipopewa utume alikuwa akiswali rakaa mbili asubuhi na jioni. Inasemekana kuwa rakaa mbili hizo ndio makusudi na mradi wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu alipomsemeza Mtume wake.

“NA UMTUKUZE MOLA WAKO NA KUMSIFU JIONI NA ASUBUHI” (40: 55)

 

DALILI YA SWALA NA TAREHE YAKE

Umethibiti ufaradhifu wa swala kwa kila muislamu ndani ya Qur-ani Tukufu, sunnah na Ijmaa.

Ama Qur-ani imeamrisha utekelezaji na swala katika makumi ya aya zake, miongoni mwake ni kauli tukufu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

”WALA HAWAKUAMRISHWA ILA KUMUABUDU ALLAH KWA KUMTAKASIA DINI (kwa ikhlaasi) WAACHE KUTOA ZAKKAH, HIYO NDIYO DINI ILIYO SAWA (98:5) Tuendelee kusoma.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *