Ukiirejea historia utangudua kuwa kuishi vema na watu au ujirani mwema aliokuwa nao Bwana Mtume ulikuwa ni sababu ya kuwavuta watu kuingia katika dini ya Mwenyezi Mungu. Bwana Mtume atuatuambia.
“Mche Mwenyezi Mungu popote (pale) ulipo na ulifuatishie baya/ovu (ulilolitenda) jema litakalolifuata(baya) na kaa/ishi na watu kwa tabia njema.” Tirmidhiy
Kuishi na watu kwa wema ni pamoja na :-
1. Kuwa mkweli katika kauli na mtendo kwa wenzio
2. Kuwa na bashasha mbele yao
3. Kuwa na shukrani kwa wema wanaokutendea
4. Kuwa wa kwanza kuwatolea salamu kila mkutanapo
5. Waite kwa majina mazuri wayapendayo
6. Wataje kwa wema
7. Wasamehe waliokukosea
8. Linda hadhi na heshima zzao
9. Usizifichue siri zao walizokueleza
10. Usijifakharishe mbele zao kwa hadhi, cheo au utajiri wako
11. Shirikiana nao kwa hali na mali katika huzuni na furaha
12. Usiwaudhi kwa kuwafanyia usilopenda wao kukufanyia
13. Waheshimu wakubwa na wahurumie wadogo
14. Wape nasaha/ushauri kwa maneno mazuri yaliyo laini unapowaona wamepotea
15. Usiwabague watu kwa sababu ya utajiri au umasikini.
Ukiishi na watu kwa kuzingatia nasaha hizi, utapendwa na jamii na utaishi katika jamii kwa furaha na amani ya kweli . Bwana Mtume -Allah anamshushie Rehema na Amani – anatuambia:-
“Miongoni mwa tabia za mitume na watu wakweli ni bashasha waonanapo na kupeana mikono wakutanapo.”