BWANA MTUME AENDA TWAIF

Kitambo kifupi baada ya Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie- na jamaa zake kutoka katika kambi ya Mzee Abuu Twaalibu ambako wali zuiliwa na kuondoshwa kwa vikwazo dhidi ya yalitokea matukio mawili ambayo yalimuathiri sana Mtume wa Mwenyezi Mwenyezi Mungu.

 Matukio haya ya huzuni si mengine bali ni ile tukio la kufiwa na Ami yake Mzee Abu Twaalib kisha kuandamiwa na kifo cha mkewe Bi Khadijah baada ya mwezi ya mwezi mmoja Mzee Abuu Twaalib aliposhikwa na maradhi na akafa kuacha hali ya uadui baina yao na Mtume akiendelea bila ya kupatiwa ufumbuzi muafaka.

Mtu pekee waliyeona kuwa ndiye mwenye mwenye ufumbuzi wa tatizo hili ni Mzee Abuu Twaalib ambaye ni kiongozi kwa upande wao na upande wa pili ni Ami na mlezi wa Mtume. Kwa hivyo wa kaamua kumuendea ili afanye suluhu kati yao na mwana wa nduguye.

Mwana sira mashuhuri Ibn Ishaq Allah amrehemu – anaelezea na kusimulia hali ilivyokuwa: (Abuu Twaalib alipozidiwa na maradhi makurayshi waliteta: Hamza na Umar wamekwishasilimu na suala la (dini ya)Muhammda limeshaenea na kutangaa katika makabila yote ya makurayshi.

Basi tumuendee Mzee Abuu Twalib atupe dhamana ya mwana wa nduguye”. Makurayshi watukufu wakaenda kawa Mzee Abuu Twaalib na kumwambia “Ewe Abuu Twaalib, hadhi yako kwetu ni kama uijuavyo, na unaiona hali uliyonayo, inatisha naunajua wazi mzozo uliopo kati yetu na mwana wanduguyo.

Basi sisi tunakuomba umuite, uchukue dhamana kwetu na kwake kwake ili yeye aache kutukera nasi tuache kumkera, yeye atuache na dini yetu na sisi tumuache nadini yake Abuu Twaalib baada ya kusikiliza kwa makini shauri waliokuja nalo jamaa zake makurayshi, akamtuam mjumbe kwenda kumuita Bwana Mtume. Mtume alipofika , Ami yake akamwambia :

“Ewe mwana wa ndugu yangu, hawa watufufu miongoni mwajamaa zako wamekusanyika kwa ajili yako ili wakupe (ahadi) nawe uwape (ahadi )”.

Bwana Mtume -Rehema naAmani zimshukie -akasema : “Ewe Ami yangu neno moja tu mlilopewa, mtawamiliki waarabu kwa neno hilo na wasio waarabu watakufuateni kwa sababu ya neno hilo”. Abu jahliaksema : “naam tuambie hata maneno kumi !” Mtume akasema Laa Ilaaha illal-laah {Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah} na mviache mnavyoviabudu kinyume cha Allah. Makurayshi wakapiga makofi (kwa kustaajabu)na wakasema:

“Ewe Muhammad, hivi unataka kuwafanya miungu wote kuwa Mwenyezi Mungu mmoja tu? Hakika jambo lsko hili ni jambo la ajabu sana! Kisha wasemezana wao kawa wao:

 ” Hakika wallah !mtu huyu {yaani Mzee Abuu Twalib} hawezi kukupeni shaurijema la kukuridhishenibasi enendeni zenu na muendelee na kuifuata dini ya baba zenu mpaka pale Mwenyezi Mungu atakapohukumu baina yenu na yeye {Muhammad}”.

 Halafu wakatawanyika.

Baada ya hapo Mzee Abuu Twaalib hakuishi muda mrefu akafariki dunia huku akifuatiwa na Bi khadijah mkewe Mtume.

Baada ya misiba miwili hii iliyompata, Mtume akawa anakabiliana ana kwa anana maadui zake bila ya kuwa na ngome na mihimili yake hii miwili ;

Ami yake na mkewe hii ndiyo fursa iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa sana na makurayshi, fursa ya ushindi dhidi ya Muhammad asiye na mtu wa kumuhami wala kumtetea.

Mzee Abuu Twaalib alikuwa ni ngome madhubuti iliyomzunguka Mtume pande zake zote na hivyo kumzuilia na kumuondoshea maudhi na madhara yote.

Ama Bi Khadijah alikuwa ni muhimili wake wandani ambapo hapo alipata utulivu na amani baada ya maudhi na makero ya makurayshi Bibi huyu mwema ndio lilikuwa kimbilio lake la pekee baada ya dhikina taabu zilompata. Alipokufa Mzee Abuu Twaalib;

Ami yake na Bi Khadijah mkewe, Bwana Mtume akwa amepatwa na misiba miwili mikubwa ambayo haikumanisha kingine zaidi ya kumpoteza msaidizi{Ami yake} na makimbilio yake {mkewe}.

Ikampata Bwana Mtume huzuni kuu kutokana na misiba hii miwili ambayo iliyofatana mpaka ukaitwa mwaka ule “mwaka wa huzuni”.

Naam, kifo cha Mzee Abuu Twaalib kilikuwa ni msiba mzito kwa Mtume kwani aliikosa ngome imara na madhubuti, kuuondoka kwa ngome hiyo ni kuwaachia mwanya na upenyo makurayshi kupambana na Mtume kwa urahisi zaidi kuliko ilivyokuwa wakati wa uhai wa ngome hiyo maudhi na kero na makurayshi kwa Mtume zikarudifika.

Kifo cha Bi Khadijah mkewe pia kilikuwa ni pigo jingine kubwa kwa Mtume, kifo hiki kiliacha pengo ambalo halikuweza kuzibika katika uhai wote wa Mtume.

Ushahidi wa hilo ni namna ambavyo Bwana Mtume alivyokuwa akimtaja sana kwa wema warehemu mkewe huyu na kuombea Mwenyezi Mungu mbeleza wakeze wengine mpaka wakawa wanafanya wivu.

Naam ni kweli lazima Mtume awe katika hali hiyo kama binadamu, nabinadamu tu bali binadamu aliyepeaw jukumu zito na gumu ; jukumu la kufikisha ujumbe wa Mola wake kwa viumbe wake.

Kwa nini isiwe hivyo, uko wapi sasa ule moyo mkubwa wenye dawa ya kumtuliza na kumliwaza baada ya tabu na ucovu anoupata katika kulitekeleza jukumu alilokabidhiwa na mola wake?!

I wapi ile akili yenye akili sambamba na uoni, akili iliyosimamamemo/makamu ya wazuri mkweli na muaminifu kwake katika shida na raha?!

Iwapi ile nafsi yenye uonakao na kila aonaye, nafsi iliyobeba mazitoyake Bwana Mtumena kushirikiana nae katika machungu yake?!

Yu wapi Khadijah, yule mkewe mwema, mtu aliyemwamini pale watu walipomkanusha na kumkataa, mtu aliyemsakisha watu walipomkabidhisha , mtu aliyemfanya kuwa mkwasi kwa mali yake akaitoa kwake yote kama alivyotoa nafsi yake?!

Li wapi anga lile la liwazo lililokuwa likimfunika kwa mapenzina huruma na kumpa nguvu mpya za kuweza kukabiliana na viziwiu na kipofu hawa wasio na akili?!

Yote haya yaliyeyuka na kuondoka kwa (na) kifo cha Bi Khadijah na Mzee Abuu Twaalib, Bwana Mtume akawa sasa hana nje mlinzi, msaidizi na hana ndani mwenye kumliwaza misba hii miwili ilikuwa ni pigo la ndani na nje.

Misiba hii ilibadilikwa muda tabia na mwenendo mzima wa Bwana Mtume,Mtume akawa ni mtu mwenye tabia ya upweke, anakaa peke yake muda mrefu na akikaa zaidi ndani bila ya kutoka nje.

Naam ilikuwa ni fursa adhimu kwa makurayshi kupambana na Mtume ana kwa ana bila ya kizuizi chotechote kweli walizidisha kero na maudhi huku wakiamini kuwa hiyo ndio njia sahihi itakayowapatia ushindi dhidi ya Mtume.

Miongoni mwa maudhi ni kama inavyosimuliwa na Imam Muslim akipokea kutoka kwa swahaba wa Mtume Ibn Masoud Allah amridhie- amesema :

siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema naAAmani alipokuwa anaswali katika Al-kaaba Huku Abu Jahli akiwa amekaa na wapambe {wafuasi}wake. Na jana yake walikuwa wamechinjwa ngamia, Abu Jahli akasema:

Nani kati yenu atakaye yaendea matumbo na uchafu wa ngamia wa baniy fulani, akyechukua akja kumuwekea Muhammad mabegani atakapokuwa amesujudu?

Akainuka mtu muovu mmmoja akaenda akayachukua nakumuwekea Mtume kati ya mabega yake. Anasema(Ibn Masoud):wakawa wanachekea na kuyumbia huku nakulanami nikiwa nimesimama ni kiangalia.

Lau ningekuwa na nguvu ningeliondosha uchafu ule mgongoni kwa Mtume wa Mwenyezi Mwenyezi Mungu.

Mtume aliendelea kusuju bila ya kunyanyua kichwa chake mpaka pale msamaria mwema alipokwenda kumpasha khabari hiyo Bi Fatmah binti ya Mtume .

Binti huyu mwema ndiye alikuja na kumuondoshea baba yake uchafu huu, kisha akawagekia mahasimu wake na kuwashutumu kutokana na kitendo chao hicho kibaya.

Mtume alipomaliza kuswali, aliwaombea dua mbaya wale wote waliofanya kitendo kile kibaya.

Hili ni moja tu miongoni mwa mrorongo mrefu wa matukio ya maudhi na kero.

Wakati mwingine makurayshi walimwagia mtume mchanga kichani, siku moja walimfuata kwenye Al-kaaba, mmojawao akmrukiana kumkaba shingo nashuka (kishali)yake kwa lengola kumnyonga mpaka afe.

Bahati nzuri aktokea swahibu yake, yule mkwerli Bwana Abuu Bakri akamsukumia mbali muoniyule, aksema il-hali akilia :

“OH! MTAMUUA MTU KWA SABABU TU ANASEMA MOLA WANGU NI ALLAH?…”[40:28]

Kwa kwelimatendoyao haya ya maudhi na kero yakikuwa na atharikubwa kwa Mtume,lau si kuwa Mwenyezi Mungu aliuthibitisha moyo wa Mtume wake na kumsaida kwa nguvu na uwezo wake, maudhi haya yalitosha kabisa kumuyumbisha Mtume na kumfitinisha na dini yake.

Hii ni miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake:

“NA HAKIKA WALIKUWA KARIBU KUKUNGEUSHA NAYALE TULUYOKUFUNULIA ILI UPATE KUTUZULIA BADALA YA HAYA (ya haki tuliyokuteremshia) NA HAPO BILA SHAKA WANGALIKUKUFANYA RAFIKI (yao mkubwa) NA KAMA TUSINGALIKUTHIBIBITISHA UNGALIKUWA KARIBU KUWAELEKEA KIDOGO. HAPO BILA SHAKA TUNGALIKUONJESHA ADHABU KUBWA YAMAISHA (ya hapa ulimwenguni na adhabu kubwa ya maisha akhera)KISHA USINGEPATA MSAIDIZIWA KUKUNUSURU JUU YETU.” [17 73-75]

 

BWANA MTUME AENDA TWAIF

Kitambo kifupi baada ya Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie- na jamaa zake kutoka katika kambi ya Mzee Abuu Twaalibu ambako wali zuiliwa na kuondoshwa kwa vikwazo dhidi ya yalitokea matukio mawili ambayo yalimuathiri sana Mtume wa Mwenyezi Mwenyezi Mungu.

 Matukio haya ya huzuni si mengine bali ni ile tukio la kufiwa na Ami yake Mzee Abu Twaalib kisha kuandamiwa na kifo cha mkewe Bi Khadijah baada ya mwezi ya mwezi mmoja.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *