HALI YA KIDINI BARA ARABU KABLA YA UISLAMU

Kabla ya kudhihiri kwa Uislamu Bara arabu halikuwa na dini moja bali lilisheheni dini nyingi. Baadhi ya wakazi wake walikuwa wakifuata dini ya Nabii Musa nao ni mayahudi na wengine waliifuata dini ya Nabii Isa, nao ni Manasara.

Mbali na hawa walikuwepo pia waliokuwa wakiyaabudia masanamu. Qur-ani Tukufu imeyataja baadhi ya masanamu yaliyofanywa miungu kama vile Laata,Uzzah, Yaghuuth, Yauuqa na Nasrah.

 Kadhalika lilikuwepo kundi dogo lililokuwa likifuata dini ya haki likimuabudu mola wa haki kupitia mafundisho yaliyoletwa na Nabii Ibrahimu kutoka kwa Mwenyezi mungu.

Mwenyezi Mungu Mtukufu alipompa utume Muhammad na kumpa kazi nzito na jukumu kubwa la kutangaza dini ya Kiislamu aliinuka na kuanza kuwalingania watu wamuabudu Mungu mmoja asiye na mshirika na waache kuyaabudu masanamu waliyoyatengeneza wao wenyewe.

Jawabu la Maquraysh lilikuwa ni kumkadhibisha Mtume na kumpinga vikali sana. Isitoshe walimuadhibu adhabu kali sana kila aliyemuamini na kumfuata Mtume ili iwe ni onyo kwa wengine.

Hawakukomea hapo tu bali waliwazuia watu kuonana na kumsikiliza Mtume lakini kwa sababu ya subira, jihadi, imani yake na msaada wa Mwenyezi Mungu alifanikiwa kuwashinda maadui wa Uislamu na kuieneza dini ya Mwenyezi Mungu miongoni mwa Waarabu na watu wa mataifa mengine.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *