MALEZI YA MTUME NA KISA CHA KIFO CHA MAMA YAKE

Mtume alifiwa na baba yake kabla hajazaliwa na hakumuachia mali ya kutosha. Mtume alipofikia umri wa miaka minne, mlezi wake na mnyonyeshaji wake Bi Haliymah alimrejesha kwa mama yake Bi Aaminah akamlea mwanawe mpaka alipofikia umri wa miaka sita akampeleka kuwazuru wajomba zake Madinah.

Bi Aminah alifia njiani wakati akirejea Makkah wakati akirejea na mwanawe baada ya ziara yake ya Madinah na akazikwa ABUWAI, kitongoji kilichoko baina ya Makkah na Madinah. Baada ya maziko ya mama yake Mtume, Mtume alichukuliwa na kupelekwa Makkah UMMU AYMANA muhabeshi.

Huyu alikuwa ni mtumishi aliyeachwa na baba yake na ndiye aliyefuatana na mama yake Mtume safarini.

Baada ya kufiwa na mama yake, Mtume alilelewa na babu yake mzaa baba Mzee Abdul Mutwalib kwa kipindi kisichopungua miaka miwili.

Babu yake alimpenda sana mjukuu wake huyu kiasi cha kumtanguliza kuliko wanawe (ami zake Mtume) na alikuwa akimketisha mahala anapokaa yeye kwa kumtukuza. Mtume alipofikisha umri wa miaka minane, babu yake alifariki dunia.

Kabla hajafariki, alimuusia mwanawe Abuu Twalib kumlea mjukuu wake, hivyo Mtume akawa chini ya uangalizi na ulezi wa Ammi yake Bwana Abuu Twalib.

Abuu Twalib alikuwa na mzigo wa familia kubwa na alikuwa na mali kidogo tu ambayo haikumtosha kuihudumia familia, lakini MwenyeziMungu akamkunjulia riziki yake kutokana na kumlea mtoto huyu yatima.

Mtume aliishi nyumbani kwa ammi yake kama mmoja wa watoto wa familia ile na alikuwa akitosheka na alichopewa; hakuwa akililia na kupupia kila alichokiona kama ilivyo tabia na ada ya watoto.

MALEZI YA MTUME NA KISA CHA KIFO CHA MAMA YAKE

Mtume alifiwa na baba yake kabla hajazaliwa na hakumuachia mali ya kutosha. Mtume alipofikia umri wa miaka minne, mlezi wake na mnyonyeshaji wake Bi Haliymah alimrejesha kwa mama yake Bi Aaminah akamlea mwanawe mpaka alipofikia umri wa miaka sita akampeleka kuwazuru wajomba zake Madinah.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *