Imempasa na kumuwajibikia mwislamu kuutwahirisha mwili, nguo, mahala/sehemu alipo na mazingira yake kwa ujumla kutokana na kila kilicho najisi kwa maana zote mbili kwani hiyo ni amri ya MwenyeziMungu alipomwambia Mtume wake bali ummah mzima :
“NA NGUO ZAKO UZISAFISHE” [74:4]
MwenyeziMungu pia amewasifia waja wake ambao hujitahidi katika suala la usafi na kujiepusha/kujilinda na najisi aliposema
“HAKIKA ALLAH HUWAPENDA WANAOTUBU NA HUWAPENDA WANAOJITAKASA” [2:22]
Katika kulisisitiza na kulitilia mkazo suala la twahara na kujiepusha na najisi Bwana Mtume anatuambia :
“Twahara ni nusu ya imani”
Kadhalika Bwana Mtume amewaagiza na kuwaamrisha wanawake kujitwaharaisha kutokana na damu ya hedhi kama alivotuamrisha sote kuondosha kila najisi.