KUMTEGEMA ALLAH

Muislamu halioni suala la kumtegema Allah katika mambo yake kulli {yote} kama ni wajibu wa kimaumbile tu, bali anaona na kuamini kuwa ni fardhi ya dini na itikadi isiyopambanuka ya Uislamu. Itikadi hii inatokana na agizo la Mola wake Mtukufu:

 “… NA MTEGEMEENI ALLAH IKIWA NYINYI NI WAUMINI.” [5:23]

“… NA WAUMINI WAMTEGEMEE ALLAH TU.” [64:13]

Amri na maagizo haya yaliyosheheni ndani ya Qurani Tukufu ndiyo yanayokufanya kumtegemea Mwenyezi Mungu mtukufu kuwe ni sehemu ya itikadi ya muislamu.

Kwa maneno mengine tunaweza kusema kuwa muislamu anapoyategemeza kusema kuwa muislamu anapoyategemeza mambo yake yote kwa Allah, huwa yumo katika kuifuta dini ya Mola wake na huwa na fungu la ajira mbele ya Allah.

Wala kumtegemea Allah si kama wanavyofahamu majahili wa uislamu kuwa ni kusema tu kwa ulimi bila ya kujishughulisha na sababu {vyanzo} vya matakwa ya mja.

Sivyo kabisa, kumtegema Allah si, kuacha kufanya kazi na ukaomba, kuridhia umasikini na kuishi maisha duni chini ya hisia za kumtegemea Allah.

Bali muislamu anafahamu kwa yakini kuwa kumtegemea Allah ambako ni sehemu ya Imani na itikadi yake, ni kumtii Allah kwa kufanya sababu zote husika ili kufikia matakwa/mahitaji yake fulani kama ni suala la riziki, basi hufanya kazi kwa juihudi na maarifa huku akiamini kuwa kazi aifanyayo ni sababu tu na mruzukaji wa kweli ni Allah pekee

“KWA YAKINI ALLAH NDIYE MTOAJI WA RIZIKI, MWENYE NGUVU, MADHUBUTI.” [51:58]

Ikiwa ni suala la elimu, basi huitafuta kwa bidii huku akiitakidi kuwa ni elimu ni wajibu wa kidini, elimu ni mali ya Allah ampayo mwanadamu:

“AMEMFUNDISHA MWANADAMU (Chungu ya) MAMBO ALIYOKUWA HAYAJUI.” [96:5]

Kama ni ugonjwa, basi hutumia dawa kwa itikadi kuywa dawa ni sababu tu ya kupona, bali mponyaji wa kweli hata bila ya kupona, bali mponyaji wa kweli hata bila dawa ni Allah pekee:

“NA NINAPOUGUA, YEYE NDIYE ANAYENIPONESHA.” [26:80]

Hii ndio dhana ya kumtegemea Allah katika uislamu, muislamu wa kweli hategemei kuvuna bila ya kupanda wala haamini kuwa kupanda ndio kuvuna, bali kupanda ni sababu tu ya mavuno apendapo Allah kwani yeye pekee ndiye muweza wa kila kitu kwa sababu unaweza kupanda na usivune:

“… NA ALLAH NI MWENYE UWEZA JUU YA KILA KITU.” [2:284]

Kauli jumla, kumtegemea Allah kwa muislamu hakumaanishi zaidi ya kufanya kazi, kutumai, kutuliza moyo na kuitakidi kwa kukata kuwa alitakalo Allah ndilo huwa na asilolitaka kamwe hilo haliwi hata kama watu wote wangelitaka, na kwamba Allah hamrejeshi patupu mwenye kumtegema kupitia sababu za kimaisha kwani kila kitu kina sababu:

“YEYE NDIYE ALIYEFANYA ARDHI IWE INAWEZA KUTUMIKA (Kwa kila myatakayo) KWA AJILI YENU. BASI NENDENI KATIKA PANDE ZAKE ZOTE NA KULENI KATIKA RIZIKI ZAKE, NA KWAKE YEYE NDIO MAREJEO (yenu nyote).” [67:15]

Muislamu anaamini utaratibu {suna} ya Allah katika ulimwengu ambayo ni kazi {juhudi} + kumtegemea Allah = matunda.

Kutokana na imani yake hii, muislamu hufanya kazi na kila linalohitajika kwa juhudi na ukamilifu ili kuyafikia malengo yake ya kimaisha.

Haitakidi hata kidogo kwamba kazi hizo anazozifanya pekee ndizo zinamdhaminia kukamilisha malengo yake na kumpatia mafanikio.

Bali huona kule kufanya sababu [kazi] ni amri na utaratibu wa Mola wake ambao hana budi kuutii kama anavyomtii katika mambo mengine anayomuamrisha kutenda au kumkataza kutenda.

Ama suala la kupata matokeo/natija ya kazi aifanyayo na kufuzu katika matakwa yake, hili analitegemeza kwa Allah, kwani yeye tu ndiye muweza wa hilo.

Wangapi wamefanya kazi ngumu za suluba na hawakupata! Hatuwaoni wakulima, waliolima, wakapanda na bado hawakuvuna!

Kutokana na hili, mtazamo wa muislamu katika sababu za kimaisha [kazi] ni kwamba kuzitegemea sababu pekee na kuziona kuwa ndio kila kitu katika kupata mahitaji ya mwanadamu ni ukafiri.

Na kwa upande mwingine mtu kuacha kufanya kazi na ilhali anao uwezo wa kufanya kazi, haya ni maasi.

Hii ndio dhana sahihi ya kumtegemea Allah kuivaa sifa hii. Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie anatuambia:

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *