JIEPUSHE NA UBAGHILI NA UNYIMI

Ewe ndugu yangu-Allah akurehemu-kwa mapenzi ya Allah ninakuusia pamoja na kuiusia nafsi yangu. Tujiepushe na tuipige teke tabia mbaya ya ubakhili na unyimi.

Viwili hivi; bakhili na unyimi si pambo na sifa ya muumini, kwani ni miongoni mwa mambo mabaya yenye kuhilikisha. Allah Mola Mtukufu anatuambia:

 “…NA WENYE KUEPUSHWA NA UBAKHILI WA NAFSI ZAO, HAO NDIO WENYE KUFAULU. MKIMKATIA ALLAH SEHEMU NZURI (katika mali zenu, mkazitoa katika njia za kheri) ATAKUZIDISHIENI NA ATAKUGHUFIRIENI. NA ALLAH NDIYE ATOAYE THAWABU NYINGI, MPOLE”. [64:16-17]

Aya inafahamisha kwamba kutokuwa bakhili ni kufaulu na kutoa katika njia za kheri ni sababu ya kuzidishiwa mali na kupata msamaha wa Allah.

Kinyume chake kuwa bakhili ni kujinyima fursa ya kufaulu kupitia mlango wa neema ya mali uliyopewa na Allah bila ya kupeleka maombi au kustahiki.

Elewa na ufahamu kwamba mali haizidi kwa kuifanyia ubakhili na ubakhili ni sababu kuu ya kukukosesha maghfira ya Allah. Zidi kutambua ewe ndugu yangu muislamu kwamba ybakhili ni shari na ni adhabu, Qur-ani Tukufu inatuambia:

“WALA WASIONE WALE AMBAO WANAFANYA UBAKHILI KATIKA  YALE ALIYOWAPA ALLAH KATIKA FADHILA ZAKE KUWA NI BORA KWAO (kufanya ubakhili huko) LA, NI SHARI (vibaya) KWAO. WATAFUNGWA KONGWA (madude ya kunasa shingoni) ZA YALE WALIYOYAFANYIA UBAKHILI SIKU YA KIYAMA. NA URITHI WA MBINGU NA ARDHI NI WA ALLAH NA ALLAH ANA KHABARI ZA (yote) MNAYOYAFANYA”. [3:180]

Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie-anatutahadharisha na ubakhili, anatuambia:

“Tahadharini/jiepusheni na ubakhili, kwani huo ubakhili ndio uliowaangamiza waliokuwa kabla yenu. (Ubakhili uliwapelekea kumwaga damu zao na kuyahalalisha waliyoharamishiwa”. Ahmad & Bukhaariy-Allah awarehemu.

Bwana Mtume anazidi kutuonya juu ya ubakhili kupitia kauli yake: “Bakhili yu mbali na Allah, yu mbali na watu, yu mbali na pepo, yu karibu mno na moto”.

Allah Mola Mwenyezi anatubainishia ndani ya kitabu chake kitukufu fadhila za kutoa na madhara (ubaya) ya ubakhili na unyimi, anasema:

“YULE ANYETOA (zaka, sadaka na vinginevyo) NA KUMCHA ALLAH. NA KUSADIKI JAMBO JEMA (akalifuata). TUTAMSAHILISHIA NJIA YA KWENDEA PEPONI. NA AFANYAYE UBAKHILI, ASIWE NA HAJA YA VIUMBE WENZAKE. NA AKAKADHIBISHA MAMBO MEMA (asiyafanye). TUTAMSAHILISHIA NJIA YA KWENDEA MOTONI. NA MALI YAKE HAYATAMFAA ATAKAPOKUWA ANADIDIMIA (motoni humo)”.     [92:5-11]

JIEPUSHE NA UBAKHILI NA UNYIMI

Ewe ndugu yangu-Allah akurehemu-kwa mapenzi ya Allah ninakuusia pamoja na kuiusia nafsi yangu. Tujiepushe na tuipige teke tabia mbaya ya ubakhili na unyimi.

Viwili hivi; bakhili na unyimi si pambo na sifa ya muumini, kwani ni miongoni mwa mambo mabaya yenye kuhilikisha. Allah Mola Mtukufu anatuambia:

 “…NA WENYE KUEPUSHWA NA UBAKHILI WA NAFSI ZAO, HAO NDIO WENYE KUFAULU. MKIMKATIA ALLAH SEHEMU NZURI (katika mali zenu, mkazitoa katika njia za kheri) ATAKUZIDISHIENI NA ATAKUGHUFIRIENI. NA ALLAH NDIYE ATOAYE THAWABU NYINGI, MPOLE”. [64:16-17]

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *