NAMNA, MAS-ALA NA MUDA WA UPAKAZI WA KHOFU

(i) NAMNA YA UPAKAZAJI WA KHOFU

Sheria haikumuachia kila mtu aitekeleze ruhusa hii ya upakazaji maji juu ya khofu kwa namna aitakayo mwenyewe, bali imeelekeza namna maalumu ya upakaji ambayo kila mtu hana budi kuifuata.

Haya sasa tufuatane pamoja tuone ni jinsi gani tunaweza kuzipakaza khofu maji:-

Mpakaji aanze kwa kuilowesha maji mikono yake (vitanga).

Halafu aweke tumbo la kitanga cha mkono wake wa kushoto chini ya kisigino cha khofu na tumbo la kitanga cha mkono wa kulia aweke kwenye ncha ya vidole (sehemu ya mbele ya khofu).

 Baada ya uwekaji huo wa vitanga ndiop akipitishe kitanga cha kulia kuelekea muundini na kile cha kushoto kuelekea ncha za vidole.

Mpakaji apakaze khofu kwa mfuo.Yaani avitawanye vidole vyake wakati wa kupaka, asivifumbe pamoja.

Kadhalika upakaji uwe ni baada ya kumaliza kutawadha viungo vingine visivyo miguu na apakaze akiwa amezivaa tayari.

 

(ii) MAS-ALA:

Lau mtu atapakaza maji juu ya khofu bila ya kupakaza chini yake, itajuzu.

Hii ni kutokana na kauli ya Imamu Aliy-Allah amuwiye radhi:

“Ingelikuwa dini hufuata rai (ya mtu) kupakaza chini ya khofu ingekuwa ni bora zaidi kupakaza chini kuliko kupakaza juu yake.” Abu Daawoud.

 

(iii) MUDA WA UPAKAZAJI:

Ruhusa ya upakazaji maji juu ya khofu imewekewa muda maalumu na sheria.

Baada ya kumalizika muda huo, ruhusa hii inabadilika.

Muda wa upakazaji unagawanyika sehemu mbili kwa kumzingatia mpakaji:-

  1. Mpakazaji mkazi yaani asiye msafiri atapakaza siku moja (masaa ishirini na nne )
  2. Mpakazaji msafiri atapakaza siku tatu (masaa sabini na mbili (72) )

Utaratibu huu wa muda unatokana na hadithi iliyopokelewa na Swaf-waan Ibn ‘Assaal – Allah amuwiye radhi – amesema:

Alituamrisha Mtume wa Mwenyezi Mungu – Rehema na Amani zimshukie – kupakaza maji juu ya khofu tutakapozivaa baada ya twahara (udhu) siku tatu tuwapo safarini na mchana na usiku (siku moja) tuwapo makazi (hatumo safarini) na janaba.

” Kadhalika tunayapata maelekezo ya muda wa upakazaji katika hadithi ya Shurayhi Ibn Haaniy – Allah amuwiye radhi – amesema:-

Nilimuuliza Bi Aysha (mkewe Mtume) – Allah amuwiye radhi – kuhusiana na upakazaji maji juu ya khofu, akasema:

(Nenda) kamuulize Aliy Ibn Twaalib, kwnai yeye ni mjuzi mno wa (mas-ala) haya kuliko mimi, kwa sababu yeye alikuwa akisafiri pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu – Rehema na Amani zimshukie. (Nikaenda) nikamuuliza akaniambia: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu – Rehema na Amani zimshukie:

“Inamjuzia msafiri kupakaza siku tatu (mchana na usiku) na mkazi siku moja (mchana na usiku). Muslim

NAMNA, MAS-ALA NA MUDA WA UPAKAZI WA KHOFU

(i) NAMNA YA UPAKAZAJI WA KHOFU

Sheria haikumuachia kila mtu aitekeleze ruhusa hii ya upakazaji maji juu ya khofu kwa namna aitakayo mwenyewe, bali imeelekeza namna maalumu ya upakaji ambayo kila mtu hana budi kuifuata.

Haya sasa tufuatane pamoja tuone ni jinsi gani tunaweza kuzipakaza khofu maji:-

Mpakaji aanze kwa kuilowesha maji mikono yake (vitanga).

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *