Maana ya nguzo.
Kabla hatujaanza kuzielezea na kuzichambua nguzo za swala moja baada ya nyingine ni vema kwanza tukajua nguzo ni nini nguzo ya kitu ni ile sehemu ya msingi ya kitu hicho kama vile kuta na msingi katika nyumba.
Kwa hivyo basi nguzo ni kile kitu cha msingi ambacho upatikanaji wa jambo/kitu Fulani unakitegema.
Rukuu na sijida, hizi ni baadhi ya sehemu za msingi zinazoijenga swala, nazo ndizo zinazoitwa nguzo za swala, swala haikamiliki wala kusihi ila kwa kutimia nguzo zake zote kwa namna na utaratibu uliopokewa kutoka kwa mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie kama nae alivyopokea kutoka kwa Jibril Amani ya Allah imshukie.
Kwa kufupi, nguzo za swala ni kumi na saba, kama ifuatavyo.