WAEPUSHE WENGINE SHARI ZAO

Muislamu unausiwa uishi na wanadamu wenzio na ujitahidi upeo wa jitihada zako shari zako zisiwafikie kwa namna yote ile iwayo.

Kwani kwa kufanya hivyo, Allah atakukinga na kukulinda na shari na maudhi yao. Tambua kwamba imethibiti kutoka kwa Bwana Mtume– Rehema na Amani zimshukie:

“Mwenye kutaka salama, basi na aitafute katika salama ya mwenziwe kutoka kwake.”

Wanuwilie kheri wanadamu wote khususan waislamu na wala usiwadhamirie shari. Wala usimfanyie undani na chuki muislamu mwenzio, bali muislamu mwema ni yule asemaye:

“…MOLA WETU! TUSAMEHE SISI NA NDUGU ZETU WALIOTUTANGULIA (kufa) KATIKA USILAMU WALA USIJAALIE KATIKA NYOYO ZETU UNDANI KUWAFANYIA WISLAMU ( wenzetu) MOLA WETU! …”  (59:10)

Ukiwa una sifa hii, huna undani wala mfundo kwa waislamu wenzako utakuwa umejijengea ngome imara dhidi ya shari zao na Allah atakuvika taji la Ucha–Mungu. Kisha ninakuusia tuuzingatie kwa pamoja wasia wa Luqmaan kwa mwanawe kama alivyousajili  Allah ndani ya Qur-ani Tukufu

“…EWE MWANANGU! USIMSHIRIKISHE ALLAH, MAANA SHIRKI NDIYO DHULUMA KUBWA.” (31:13) Akaendelea kumuusia:

“EWE MWANANGU! KWA HAKIKA JAMBO LO LOTE LIJAPOKUWA NA UZITO WA CHEMBE YA HARDALI, LIKAWA NDANI YA JABALI AU MBINGUNI AU KATIKA ARDHI, ALLAH ATALILETA (amlipe aliyefanya) BILA SHAKA ALLAH NI MJUZI WA MAMBO YALIYOFICHIKANA (na) MJUZI WA MAMBO YALIYO DHAHIRI. EWE MWANANGU! SIMAMISHA SWALA, NA UAMRISHE MEMA NA UKATAZE MABAYA, NA USUBIRI JUU YA YALE YATAYOKUSIBU (kwani mwenye kuamrisha mema na kukataza mabaya lazima zitamfika tu taabu) HAKIKA HAYO NI KATIKA MAMBO YANAYOSTAHIKI KUAZIMIWA (na kila mtu) WALA USIWATAZAME (usiwafanyie watu jeuri) KWA UPANDE MMOJA WA USO, WALA USENDE KATIKA NCHI KWA MARINGO, HAKIKA ALLAH HAMPENDI KILA AJIVUNAE, AJIFAKHIRISHAYE NA USHIKE MWENDO WA KATIKATI, NA UTEREMSHE SAUTI YAKO, BILA SHAKA SAUTI YA PUNDA NI MBAYA KULIKO SAUTI ZOTE (kwa  makelele yake bure)”  (3:16-19)

Ninazidi kukuusia ewe ndugu yangu mpenzi pamoja na kuiusia nafsi yangu ya kwamba tuwe miongoni mwa waja wa Rahmaani–Allah mwingi wa rehema:

“….AMBAO WANAOKWENDA (na kurejea) ULIMWENGUNI KWA UNYENYEKEVU, NA WAJINGA WAKISEMA NAO (maneno mabaya) HUWAJIBU (maneno ya) SALAMA NA WALE WANAOPITISHA BAADHI YA SAA ZA USIKU KWA AJILI YA MOLA WAO KWA KUSUJUDU NA KUSIMAMA NA WALE WANOSEMA MOLA WETU! TUONDOLEE ADHABU YA JAHANAMU, BILA SHAKA ADHABU YAKE NI YENYE KUENDELEA NA WALE AMBAO WANAPOTUMIA HAWATIMII KWA FUJO WALA HAWAFANYI UBAKHILI, BALI WANAKUWA KATIKATI BAINA YA HAYO. NA WALE WASIOMUOMBA MUNGU MWINGINE PAMOJA NA ALLAH, WALA HAWAUI NAFSI ALIYOIHARIMISHA ALLHA ISIPOKUWA KWA HAKI, WALA HAWAZINI, NA ATAKAYEFANYA HAYO ATAPATA MADHARA (papa hapa ulimwenguni kabla ya Akhera).” (25:63–68)

Na tuwe katika:

“…WALE AMBAO HAWASHUHUDII SHAHADA ZA UWONGO, NA WANAPOPITA PENYE UPUUZI, HUPITA KWA HISHIMA (yao) NA WALE AMBAO WANAPOKUMBUSHWA AYA ZA MOLA WAO HAWAZIANGUKII KWA UZIWI NA UPOFU. NA WALE WANAOSEMA: MAOLA WETU! TUPE KATIKA WAKE ZETU NA WATOTO WETU YABURUDISHAYO MACHO (yetu, nyoyo zetu) NA UTUJAALIE KUWA WAONGOZI KWA WAMCHAO ALLAH”.  (25:72-74)

Ewe ndugu yangu katika imani-Allah akurehemu-elewa na ufahamu kwamba tukiushika wasia huu na tukajipamba na sifa hizi. Basi hapana shaka kwamba tutakuwa ni malaika watembeao katika ardhi na ujira adhimu unatungojea kesho mbele ya Allah:

“…HAO (wenye sifa hizo) NDIO WATAKAOLIPWA GHOROFA (za peponi) KWA KUWA WALISUBIRI, NA WATAKUTA HUMO HISHIMA NA AMANI. WAKAE HUMO MILELE, KITUO KIZURI NA MAHALA PAZURI (kabisa) PA KUKAA”. (25:75–76)

Tuusiane na tutambue kuwa gharama na thamani ya kununulia hizo ghorofa za peponi ambazo ni mahala pazuri mno pa kukaa mja ni kuishi katika ulimwengu huu kwa kujipamba na sifa tulizozitaja. 

Mola wetu Mtukufu tunamuomba atujaalie kwa fadhila zake kuwa ni miongoni mwa “WAJA WA RAHMAANI” – Aamiyn!

 

WAEPUSHE WENGINE SHARI ZAKO

Muislamu unausiwa uishi na wanadamu wenzio na ujitahidi upeo wa jitihada zako shari zako zisiwafikie kwa namna yote ile iwayo.

Kwani kwa kufanya hivyo, Allah atakukinga na kukulinda na shari na maudhi yao. Tambua kwamba imethibiti kutoka kwa Bwana Mtume– Rehema na Amani zimshukie:

“Mwenye kutaka salama, basi na aitafute katika salama ya mwenziwe kutoka kwake.”

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *