VITA VYA FUJJAAR NA VIAPO VYA NUSRA

Bwana Mtume – Rehma na Amani zimshukie – alijenga moyo wa kushirikiana na jamii yake katika kazi zote za ujenzi wa jamii yake kama tulivyoona namna alivoshiriki katika ujenzi wa Al-Kaaba.

Kwa upande mwingine alikuwa akichukia sana kushirikiana nao katika zile ada na desturi mbaya japokuwa jamaa zake walitamani ashirikiane nao lakini mara zote alikuwa akiwakatalia.

Vita vya “Fujjaar” ni ushahidi tosha uonyeshao jinsi Mtume Muhammad alivyoshirikiana na jamii yake.

Alipofikia umri wa miaka kumi na tano au ishirini alijiunga na jamii yake katika vita vya Fujjaar.

 Sababu ya vita hivi ilikuwa ni kulinda na kuhifadhi heshima na utukufu wa ile miezi minne mitukufu iliyotajwa ndani ya Qurani ambamo vita vimeharamishwa.

Mojawapo la makabila ya Hijazi ilivunja utukufu wa miezi ile kwa kulishambulia kabila jingine ndani ya miezi ile mitukufu, ndipo makabila mengine yakajiunga pamoja kuliadabisha kabila lile chokozi.

Kazi ya Bwana Mtume katika vita hivi ilikuwa ni kuwakusanyia silaha wapiganaji na wakati mwingine ilimbidi kushiriki moja kwa moja katika medani ya vita.

Vita hivi vilidumu kwa kipindi kisichopungua miaka minne, vikaisha kwa kuwekeana mkataba wa suluhu na amani baina ya zile pande mbili husika huku upande wa uliopoteza idadi kubwa ya watu ukilipwa fidia na upande mwingine.

Viapo vya Nusura : hili ni tukio lililotokea wakati Mtume Muhammad akiwa na umri wa miaka ishirini.

Viapo vya nusra ilikuwa ni mojawapo ya maazimio ya kikundi cha kutetea haki ambacho kimsingi ilikuwa ni kumtetea mtu mnyonge asidhulumiwe, kumpatia haki kila mwenye kuistahiki na kumsaidia kila mwenye haja na matatizo.

Maazimio ya kikundi hiki yalipitishwa ndani ya nyumba ya Bwana Abdillah bin Jad’aan Al-Tamiymi, huyu alikuwa miongoni mwa viongozi wa makurayshi .

Mtume Muhammad aliona hii ndio fursa aliyoitamani na kuingojea kwa muda mrefu ili aweze kushirikiana na jamii yake katika kuyapiga vita maovu na dhuluma iliyoitawala jamii yake.

Hivyo basi kutokana na azma hiyo alishiriki kikamilifu na ami zake katika kikao kile na kuwa miongoni mwa walioshiriki kuyapitisha maazimio yale matukufu.

VITA VYA FUJJAAR NA VIAPO VYA NUSRA

Bwana Mtume – Rehma na Amani zimshukie – alijenga moyo wa kushirikiana na jamii yake katika kazi zote za ujenzi wa jamii yake kama tulivyoona namna alivoshiriki katika ujenzi wa Al-Kaaba.

Kwa upande mwingine alikuwa akichukia sana kushirikiana nao katika zile ada na desturi mbaya japokuwa jamaa zake walitamani ashirikiane nao lakini mara zote alikuwa akiwakatalia.

Vita vya “Fujjaar” ni ushahidi tosha uonyeshao jinsi Mtume Muhammad alivyoshirikiana na jamii yake.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *