NGUZO ZA KIISLAMU

Dini hii ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo tatu za msingi, ambazo ni:-

1.         UISLAMU, ambao huu umejengwa juu ya nguzo     tano kama zifuatavyo:-

  1. Shahada mbili
  2. Kusimamisha swala tano
  3. Kutoa zakah
  4. Saumu ya Ramadhani
  5. Kuhiji Makah (kwa mwenye uwezo).

2.         IMANI nguzo hii  ya pili ya dini ya Kiislamu inajengeka juu ya nguzo sita zifuatazo:-

1.                  Kumuamini  Allah

2.                  Kuwaamini malaika wa Allah.

3.                  Kuviamini vitabu vya Allah.

4.                  Kuwaamini mitume (wote ) wa Allah.

5.                  Kuamini siku ya mwisho.

6.                  Kuamini qadari ya Allah (ya kheri au ya shari) kuwa inatoka kwa Allah).

 

3.         IHSANI. Nguzo hii ya tatu inaundwa na nguzo hii:-

Kumuabudu Allah kama unamuona Kama humuoni yeye anakuona wewe.

Huu kwa muhtasari ndio Uislamu, dini na mfumo sahihi na kamili wa maisha kwa wanadamu wote waliochaguliwa na Allah Mola Muumba wao:

“………LEO NIMEKUKAMILISHENI DINI YENU NA KUKUTIMIZIENI NEEMA YANGU NA NIMEKUPENDELEENI UISLAMU UWE DINI YENU ………….” (5:3)

elewa na ufahamu kwamba kuishi nje ya dini hii ni kulikana umbile lako kwani UISLAMU NI HAKI YAKO YA KUZALIWA uliyopewa hadiya (zawadi) na Mola Muumba wako.

6 thoughts on “NGUZO ZA KIISLAMU

  1. Asalaam aleyqum warahmatullah wabarakatuh naona waislam hatutaki kuijua dini yetu miaka nane hakuna hata aliekoment jmn allah atakulipa ujira mwema mimi nitaisoma nitandika nihifadhi ilizinisaidie kujua dini yamgu alh

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *