IBADA YA MASANAMU

Kabla ya Uislamu waarabu walizama mno katika ibada ya masanamu mpaka wakaijaza Al-Kaaba masanamu ambayo idadi yake ilifikia masanamu mia tatu na sitini (360).

Kila kabila lilikuwa na sanamu lake pekee na kila kaya/familia ilikuwa na sanamu malum kwa ajili ya familia hiyo tu.

Mtu alipotaka kusafiri, alilichukua safarini sanamu moja ilikufanikiwa safarini na walikuwa wakiyatakasa na kuyatukuza masanamu haya kiasi cha kuyatolea Qurubaani na dhabihu (sadaka za kuteketeza).

Waarabu walipokuwa wakitaka ushauri katika mambo yao mfano ndoa, biashara au safari basi uliendea “Hubal” sanamu lililokuwa ndani ya Al-kaaba wakampa ngamia na dir-ham mia mshika kete ambazo moja ilikuwa imeandikwa juu yake maneno”Mungu wangu amenikataza” na ya pili “Mungu wangu ameniamrisha” ya tatu “Naam/Ndiyo” ya nne “Hapana“.

 Jumla kete zilikuwa ni saba, mshika kete huzizungusha na kuzichanganya kisha akaitoa moja na kilichoandikwa juu yake ndio huwa amri iliyotoka kwa Mungu sanamu.

IBADA YA MASANAMU

Kabla ya Uislamu waarabu walizama mno katika ibada ya masanamu mpaka wakaijaza Al-Kaaba masanamu ambayo idadi yake ilifikia masanamu mia tatu na sitini (360).

Kila kabila lilikuwa na sanamu lake pekee na kila kaya/familia ilikuwa na sanamu malum kwa ajili ya familia hiyo tu.

Mtu alipotaka kusafiri, alilichukua safarini sanamu moja ilikufanikiwa safarini na walikuwa wakiyatakasa na kuyatukuza masanamu haya kiasi cha kuyatolea Qurubaani na dhabihu (sadaka za kuteketeza).

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *