KWA NINI DINI? (UMUHIMU WA DINI KATIKA MAISHA YA MWANADAMU)

Ingawa katika ulimwengu huu tuishimo kuna watu wanaoutaka ulimwengu uelewe kuwa mahitaji makuu ya msingi ya mwandamu ni maskani (nyumba), mavazi na chakula.

Yaani ili mwanadamu aweze kuishi katika ulimwengu huu ni lazima apate vitu hivi.

Ni sawa kwa kiwango Fulani kusema hivi lakini hili halizuii ukweli kwamba mwanadamu anaweza kuishi kwa muda Fulani bila ya vitu hivi vyote.

Hata hivyo mwanadamu hana namna ya kuepa kuishi bila ya kufuata dini yeyote japo kwa sehemu ya sekunde.

Ukweli huu unatokana na dhana hai kwamba hakuna mwanadamu anayeishi bila ya kufuata mfumo fulani wa maisha.

Uwe mfumo huo ni ule uliobuniwa na wanadamu wenyewe kwa ajili ya jamii Fulani (mfumo binadamu). Au ni ule aliochaguliwa mwanadamu na Mungu Muumba wake.

Kwa hivyo, tutaona kwamba mwanadamu ni kiumbe mwenye maumbile yanayomlazimisha kufuata mfumo fulani katika kuyaendea maisha yake ya kibinafsi sambamba na yale ya kijamii. Kwa mantiki hii hatuna namna ya kuepa kusema kuwa mwanadamu hawezi kuishi bilaya dini, bila ya kujali usahihi au ubatili wa dini hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *