KATAZO LA WIKI (JUMA LA 78)

Kwa nini lakini unamfanyia husda na kumchukia mwenzako kwa sababu tu ya neema ya mali aliyo nayo?! Kwani wewe hutambui kwamba hiyo ni mipango yake Allah kumpa huyu zaidi, yule kidogo na mwingine akamnyima?!

Acha, huko ni kuingilia utendaji wa Mgawa riziki, kwani wewe hujui kwa nini huyo amempa kingi, wewe kidogo na yule akampa kiduchu.

Hebu na tuizingatie pamoja kauli ya Mwenye riziki yake: “Na Allah amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine katika riziki. Na wale walio fadhilishwa hawarudishi riziki zao kwa wale ilio wamiliki mikono yao ya kulia ili wawe sawa katika riziki hiyo. Basi je, wanazikataa neema za Allah?” An-Nahli [16]:71

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *