MAANA YA DINI

Wanadamu kama viumbe waliotofautiana katika maumbile (sura), lugha, rangi, hali za kimaisha, fikra na kadhalika.

Wameielewa “dhana dini” kwa maana mbalimbali. Maana hizi ukizingatia kwa fikra za haraka haraka, fikra za kijuu juu zisizochimba na kupenya ndani.

Utaona kuwa zinatofautiana, lakini ukweli na hakika ni kwamba zinaona na kuhusiana kwa namna moja au nyingine hii ni kwa sababu zote zinachimbuka kutoka katika chemchem moja ambayo ni akili ya mwanadamu.

Sasa basi ukizijumuisha na kuziunganisha pamoja maana hizo, hatimaye utatoka na natija ya mwisho kwamba kumbe dini kama aielewayo mwanadamu ni:

(Mfumo/utaratibu Fulani wa maisha unaofuatwa na jamii Fulani ya wanadamu).

Hili ndilo eleweko la dhana dini kupitia akili, fikra na mawazo ya binadamu.

Sasa basi ili kuutambulisha kwa walimwengu mfumo wa maisha aufuatao mwanadamu akaamua kuupa jina mfumo wake huo aliojichagulia na kuufuata.

Unaweza kuukuta mfumo huo chini ya majina kama  mila/desturi/utamaduni, au ujamaa, ukomunisti, ubepari, kutoamini kuwepo kwa Munguu (Atheism), ushirikina (Polytheism) na kadhalika.

Hii yote ni miongoni mwa mifumo hai ya maisha inayofutawa na matabaka Fulani ya watu wanaounda jamii ya wanadamu katika ulimwengu huu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *