RIYAA

“Riyaa” ni miongoni mwa tabia mbaya ambazo muislamu anatakiwa bali anawajibika kujiepusha nayo ili aweze kufikia uhalisi na ukamilifu wa ibada zake.

Riyaa ni maradhi hatari ya moyo, kirusi hiki hatari huishambuliwa ikhlasi na kuiondosha kabisa katika moyo wa mja.

Mja akikosa ikhlasi huwa amekosa bima (kinga) ya ibada zake na hivyo kutoa mwanya wa kushambuliwa ibada zake hizo na mdudu mbaya “riyaa”.

Riyaa ina athari mbaya kwa mja kwani itazifanya ibada zake hizo siku ya kiama itafanya kama mavumbi yapeperushwayo na upepo.

Riyaa itamfanya mtu awe muflis awe hana malipo yoyote mbele mola wake.

Hapa ndipo unajitokeza umuhimu wa kuibainisha tabia hii mbaya ili Muislamu aijue na akishaijua aiepuke upeo wa uwezo wake.

Hebu sasa na tujiulize “riyaa” ni nini ili tuweze kufuatana pamoja.

Riyaa” hii ni isimu (nomino) itakanayo na lugha ya kiarabu. Isimu hii ya “riyaa” ikatafsiriwa kuwa ni kufanya abada (amali njema) kwa lengo la kuwaonyesha watu ili :

– uonekane kuwa ni mwema kuliko ulivyo

– upate kupendeza machoni mwao

– upate maslahi fulani kutoka kwao (mali au cheo)

Kwa ibara sahihi tunaruhusika kusema kuwa “riyaa” ni kufanya ibada kwa ajili tu ya kuwaonyesha watu na si kwa ajili ya Allah: hiyo ndiyo tabia mbaya ya riyaa tunayokusudia hapa kwa lengo la kukutanabaisha ili uweze kuiepuka maana hiyo ya riyaa unaweza kuiona kwa kuipitia kauli ya Allah:

” NA AMBAO WANATOA MALI ZAO KWA KUONYESHA WATU (riyaa) WALA HAWAAYAMINI (aliyoyasema) ALLAH WALA SIKU YA MWISHO……(4:38)

“…. NA WANAPOSIMAMA KUSWALI HUSIMAMA KWA UVIVU, WANAONYESHA WATU (kuwa wanaswali) WALA HAWAMTAJI ALLAH HATA KIDOGO ” (4:142)

Riyaa ni kinyume cha ikhlasii, kwa kweli huu ni dharura kuwa pasipo na ikhlaswi pana riyaa tu na si vinginevyo na palipo na riyaa bila shaka hapana ikhlaaswi hapo.

Muislamu hafanyi ibada zake kwa riyaa wala riyaa si sifa yake, bali muislamu hufanya ibada zake zote kwa ikhlaswi akiiteekeza amri ya mola wake:

” WALA HAWAKUAMRISHA ILA KWA KUMUABUDU ALLAH KWA KUMTAKASIA DINI (ikhlaswi)….” (98:5)

“SEMA MOLA WANGU AMEAMRISHA UADILIFU NA (ameniambia nikuambieni) ELEKEZENI NYUSO ZENU(kwake) WAKATI WA KILA SWALA NA MWABUDU YEYE TU KWA UTII HALISI (ikhlaswi)….” (7:29)

Muislamu hujiepusha na riyaa kwa sababu anamini kuwa kumfanya riyaa ni kumshirikisha Allah kwa mujibu wa kauli ya mtume wa Allah rehma na amani zimshukie:

” uchache wa riyaa ni shirika ….” Ibn Maajah, Al Hakim na Bayhakiy.

Inamtosha Muislamu kuona ubaya ya maradhi haya hatari ya riyaa na kujiepusha nayo kwa kupata chanjo ya ikhlaswi, kuwa Allah na mtume wake wanaichukia riyaa na Allah amewaandalia adhabu kali wale wote wafanyao amali zao kwa riyaa tusome:

“BASI ADHABU ITAWATHUBUTIKIWA WALE WANAOSALI AMBAO WANAPUUZA (maamrisho ya) SWALA ZAO;AMBAO HUFANYA RIYAA (hufanya amali zao ili watu wawaone tu)” (107:4 – 7)

Mwenye kufanya riyaa katika amali zake huwa hana chembe ya ujira wa amali hizo mbele ya Allah zaidi ya kuonekana na hao anaowaonyesha amali zake na kumjazia sifa kwa makilo.

Riyaa ni sababu ya kubatilika amali (ibada) ya mja kama inavyobainisha kaili hii tukufu ndani ya kitabu kitukufu:

” ENYI MLOAMINI MSIBATILISHE (thawabu za) SADAKA ZENU KWA MASUMBULIZI YA UDHIA KAMA YULE ANAYETOA MALI YAKE KWA KUJIONESHA MBELE YA WATU (riyaa) WALA HAMUAMINI ALLAH, WALA SIKU YA MWISHO. BASI HALI YAKE NI KAMA HALI YA JABALI AMBALO JUU YAKE KUNA UDONGO, KISHA IKALIFIKIA (jabali hili) MVUA KUBWA (ikasukuma udongo wote huo) NA IKALIACHA TUPU. BASI HAWATAKUWA NA UWEZO (wa kupata) CHOCHOTE KATIKA WALIVYOVICHUMA NA ALLAH HAWAONGOZI WATU MAKAFIRI” (2:264)

Allah Subhanahu Wata’alah haitaki wala hana haja na amali yoyote ambayo mja ataofanya kwa kumshirikisha yeye na viumbe.

Hivi ndivyo anatuambia katika hadithi-qudsi :”atakayefanya amali na akamshirikisha mwingine (asiye mimi) katika amali hiyo. basi amali hiyo ni yake yote (huyu mwingine) nami hujitenga mbali nayo (amali hiyo), nami mkwasi kuliko wakwasi wote na shirika.” Muslim.

Riyaa ni adui mkubwa wa ibada na amali yako yote, ili kubainisha ubaya wake, Bwana Mtume rehma na amani zimshukie akiita kuwa ni “shirki ndogo” akasem:

HAKIKA NILICHELELEALO (niliogopeayo) KWENU KULIKO YOTE NI SHIRKI NDOGO. (maswahaba) WAKAMUULIZA: EWE MTUME WA ALLAH-NI IPI HIYO SHIRKI DOGO? AKAMJIBU NI RIYAA, Mwenyezi Mungu mtukufu atasema siku ya kiama atakapokuwa anawalipa waja (wake) kwa mujibu wa amali zao: waendeni wale mliokuwa mkiwaonyesha amali zenu ulimwenguni, muone kama mtapata malipo (jazaa) kwao“.

SURA (MAENEO) ZA RIYAA:

Riyaa hujidhihirisha katika sura kadhaa, tutazibainisha baadhi ya surah hizo ili mtu asije akatumbukia ndani ya janga hili bila ya kujijua.

1) Mja kuzidisha twaa, pale anaposifiwa mfano anaposoma quran watu wakamsifia kama anasoma vizuri hapo hupata kichwa na kuzidisha kusoma kwa juhudi, za makusudi ili kuwaonyesha watu kuwa yeye ndiye mwenyewe kwa usomaji wala kama yeye hapana. Hufanya hivyo akilenga kuzidi kusifiwa.

Hii ni riyaa jitahidi kuiepuka kwani haina faida hata kidogo nawe.

2) mtu kuwacha kufanya ibada au amali yoyte ya kheri kwa sababu amekosolewa katika utendaji wake au hakusifiwa.

Kuacha kuendelea na amali ya twaa, eti kwa sababu hakusifiwa hiyo ni ushahidi dhahiri kuwa hamkumsudia Allah-mlipaji bali viumbe wasio na cha kukulipa. Hii ni sehemu ya maradhi ya riyaa jikinge nayo.

3) kufanya ibada kwa nguvu bidii, furaha na nyeyekevu mkubwa anapokuwa mbele ya watu lakini anapokua pekee ibada ile ile huifanya kwa uvivu na haraku haraka kama mtu amelazimishwa.

Hii pia ni riyaa inaonyesha dhahiri kwamba amali yako hiyo huwa unaifanya ili upate kuambiwa kwamba wewe ni mcha Mungu na hao wanaokuzunguka wakati huo lakini unapokua faraghani wewe na mola wako pekee hufanyi ibada kama vile unavyofanya mbele ya watu

4) mtu kutoa sadaka katika mazingira ambayo lao asingekuwepo mtu fulani watakao muona akitoa, basi asingelitoa hiyo nayo riyaa kwa sababu hutoi kwa ajili ya mola wako bali unatoa ili uonekane na akina fulani. Watakusaidia nini hao kina fulani mbele ya Allah?

“KWA YAKINI HAO HAWATAKUFAA LOLOTE MBELE YA ALLAH……” (45:19)

5) mtu kusema maneno ya haki au ya kheri au kutenda matendo mema ambayo dhahiri yake ni kuwa anafanya kwa ajili ya Allah, na hivo ndivyo watu wanavyomuona kwa sababu anajitokeza mbele ya watu lakini batini yake sivyo hivyo yeye anayafanya yote haya kama ngazi tu ya kupatia haja zake kwa watu. Hii pia ni riyaa tahadhari nayo.

Hii ndiyo riyaa, adui wako atakayekufanya wewe uwe muflis siku ya kiama kama hujamkana na kumuepuka leo. Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah- Allah amiwiye radhi. Amesema :

nilimsikia Mtume wa Allah rehma na amani zimshukie amesema “mtu wa mwanzo atakayehukumiwa siku ya kiama ni mtu aliyeuwawa shahidi. (ataletwa mbele ya Allah) na atamtambulisha neema zake alizomneemesha nazo duniani nae azitambue (neeme hizo) kisha amuambie umefanya nini kwa neema hizo nilizokupa?

Atajibu: nilipigania dini yako mpaka nikafa shahidi. (Allah) atamuambia umeogopa wewe ulipigana ili uambiwe wewe ni jasiri, na ulikwishaambiwa (ulishalipata hilo).

 Kisha ataamrishwa akokotwe kiusouso mpaka motoni.(na atakayehukumiwa mwanzoni ni) mtu aliyejfunza elimu na akaifundsha na akasoma Quran atamleta na atamtambulisha neema zake nae atazitambua.

Kisha amuambie: umefanyia nini neema hizo?akajibu: nilijifunza elimu na nikaifundisha elimu na nukasoma Quran kwa ajili yako. (Allah) atamuambia: umeogopa, wewe ulijifunza elimu ili uambiwe mwanachuoni (una elimu) na ulisoma Quran ili uambiwe msomaji na yote hayo ulishaambiwa

kisha ataamrishwa akokotwe kiusouso mpaka motoni, na mtu ambaye Allah amemkunjulia namna kwa namna za mali ataletwa na atamtambulisha neema zake naye azitambue, atamuuliza; umefanya nini kwa neema hizi atajibu: sikuiacha njia yoyoyte unayopenda mtu atoe katika (njia) hiyo ila nilitoa.

Atamuambia: umeongopa, wewe ulifanya yote hayo ili uambiwe kuwa ni karimu na tayari ulishaambiwa. Kisha atamuamrisha aburuzwe kiusouso mpaka motoni” muslim.

 

RIYAA

“Riyaa” ni miongoni mwa tabia mbaya ambazo muislamu anatakiwa bali anawajibika kujiepusha nayo ili aweze kufikia uhalisi na ukamilifu wa ibada zake.

Riyaa ni maradhi hatari ya moyo, kirusi hiki hatari huishambuliwa ikhlasi na kuiondosha kabisa katika moyo wa mja.

Mja akikosa ikhlasi huwa amekosa bima (kinga) ya ibada zake na hivyo kutoa mwanya wa kushambuliwa ibada zake hizo na mdudu mbaya “riyaa”.

Riyaa ina athari mbaya kwa mja kwani itazifanya ibada zake hizo siku ya kiama itafanya kama mavumbi yapeperushwayo na upepo.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *