MALI NA NAMNA YA KUITUMIA

Hii pia ni miongoni mwa tabia njema ambazo muislamu anapaswa kujijpamba nazo kuhusiana na hili tunasoma:

NA UMPE JAMAA (YAKO) HAKI YAKE NA MASIKINI NA MSAFIRI ALIYEHARIBIKIWA, WALA USITAWANYE (mali yako) KWA UBADHIRIFU.” [17 : 26]

 Tuzidi kusoma kwa kutafakari:

“WALA USIFANYE MKONO WAKO (kama) ULIOFUNGWA SHINGONI MWAKO, WALA USIUKUNJUE OVYO OVYO, UTAKUWA NI MWENYE KULAUMIWA (ukifanya hivyo) NA KUFILISIKA (ukiukunjua ovyo ovyo). “[17:29]

Kwa mujibu wa aya muislamu si mtu mbadhirifu na pia si bakhili. Aya hizi ndizo zinazoibeba sera nzima ya mali na namna ya kuitumia katika uislamu.

Muislamu anaamini kuwa Allah ndiye muumba wake na ndiye aliyemuumbia ulimwengu na vyote vilivyomo ndani yake ikiwa ni pamoja na mali:

“YEYE NDIYE ALIYEKUUMBIENI VYOTE VILIVYOMO KATIKA ARDHI (kabla hajakuumbeni ili mkute kila kitu tayari) – – -.” [2 : 29]

Na akamfanyia mali kuwa ni pambo la maisha yake hapa duniani:

“MALI NA WATOTO NI PAMBO LA MAISHA YA DUNIA —.” [18 : 46] Hii ndio sababu tunaona kuwa ni tabia bali ni maumbile ya mwanadamu kuipenda mali: “NA MNAPENDA MALI PENDO LA KUPITA KIASI.” [89 : 20]

“WATU WAMETIWA HUBA YA KUPENDA WANAWAKE NA WATOTO NA  MIRUNDI YA DHAHABU NA FEDHA NA FARASI WANAOTUNZWA VIZURI NA WANYAMA NA MASHAMBA NA HAYO  NI MATUMIZI YA MAISHA YA DUNIA NA KWA ALLAH NDIKO KWENYE MAREJEO MAZURI” (3:14)

kwa kuwa tayari Qur-ani tukufu imeshatuthibishia kwamba ni sehemu ya maumbile ya mwanadamu kupenda mali, ndipo tunamuona huyu mwanadamu akiitafuta na kujilimbikizia mali kwa hila, mbinu na juhudi za upeo wake.

Anachokijua yeye ni kupata mali na kuitumia bila ya kujali anaipataje na anaitumiaje. Muislamu hawi hivi kwa sababu anatambua

“KISHA KWA HAKIKA MTAULIZWA SIKU HIYO JUU YA NEEMA (mlizopewa mlizitumiaje)” (102:8)

Muislamu anaitakidi kwamba mali kwa dhati yake yenyewe kama mali haina thamani wala ubora bali thamani na ubora wake unajidhihirisha katika matumizi yake. Ni matumizi haya ndio huzaa manufaa, faida na kumletea ustawi na maslahi mwanadamu.

Manufaa na faida hizi ndizo humpelekea mtu kuipenda mali na kuhangaika kuitafuta kwa udi na uvumba.

Uislamu haumkatazi muislamu kuitafuta na kuimiliki mali bali   unachokiangalia na kukisisitiza ni namna ya kuchuma na jinsi ya kuitumia:

 “NA UTAFUTE KWA YAKE (mali) ALIYOKUPA ALLAH MAKAZI MAZURI YA AKHERA, WALA USISAHAU SEHEMU (fungu) YAKO YA DUNIA NA UFANYE WEMA KAMA ALLAH ALIVYOKUFANYIA, WALA USITAFUTE KUFANYA UFISADI KATIKA NCHI, BILA SHAKA ALLAH HAWAPENDI MAFISADI” (28:77).

Kupitia aya hii hatutashindwa kuona kuwa mali imekusudiwa imnufaishe mwanadamu katika maisha haya ya ulimwengu huu, ale, anywe, avae na alale, mahala pazuri bila ya kufanya ubadhilifu

”……NA KULENI (Vizuri) NA KUNYWENI (vizuri) LAKINI MSIPITE KIASI TU. HAKIKA YEYE (Allahl) HAWAPENDI WAPITAO KIASI (7:31).

Kadhalika aitumie mali kwa kuyanunua maisha ya milele ya akhera kwa kuitumia katika njia za kheri zitakazomuhakikishia manufaa kwanza yeye mwenyewe binafsi na jamii nzima ya wanadamu.

Aitumie namna hii ya mali aliyoneemeshwa na kuchaguliwa kupewa na Mola na sio kwa uhodari wake, juhudi wala elimu yake kwa kukidhi haja zake binafsi za kimaisha, familia yake khasa na jamii kwa ujumla.

Aitumie kuwasaidia ndugu, jamaa, marafiki, majirani, wagonjwa na wasiojiweza bila ya kuwasahau mayatima.

Awape  huku akiamini kuwa ni haki yao kutoka kwa Mola wao na sio ihsani na msaada kutoka kwake ambao atautoa akitaka na kumpa amtakaye yeye:

“……NA WAPENI KATIKA MALI YA ALLAH ALIYOKUPENI………” (24:33).

Hii ndio nadharia (dhana)  ya mali katika Uislamu, ni sehemu ya imani ya muislamu kuamini kwamba kila kilichomo mikononi mwake ikiwa ni pamja na yeye mwenyewe ni miliki yha Allah:

(vyote) VILIVYOMO MBINGUNI NA VILIVYOMO ARDHINI NI VYA ALLAH……(2:284)

Mwanadamu atakapoitumia mali yake katika mambo ya kheri na akaisaidia jamii, basi bila ya shaka atakuwa ni kipenzi cha jamii hiyo kwani ni maumbile ya mwanadamu kumpenda muhisani wake na kumchukia bakhili.

 Ziada ya hayo atapendwa na Mola wake, Mwenye mali yake:

 “…….NA ALLAH ANAWAPENDA WAFANYAO WEMA / IHSANI (3: 134).

Uislamu haukumkataza muislamu kutafuta  na kumiliki mali lakini pia haukumruhusu kuwa mbadhirifu:

”……..WALA USITAWANYE (mali yako) KWA UBADHILIFU. HAKIKA WATUMIAO KWA UBADHILIFU NI NDUGU WA MASHETANI (wanamfuata shetani)…….” (17:26-27) wala haukumuhalalisha ubakhili:

”……BILA SHAKA ALLAH HAWAPENDI WENYE KIBURI WAJIVUNAO AMBAO HUFANYA UBAKHILI (wao) NA HUWAAMURU WATU (wengine) NA WANAYAFICHA ALIYOWAPA ALLAH KWA FADHILA ZAKE………” (4:36-37).

Zidi kuona ubakhili usivyokuwa na nafasi  katika mfumo sahihi wa maisha unaowafaa wanadamu wa rangi, lugha na zama zote:

“NA AFANYAJE UBAKHILI, ASIWE NA HAJA NA VIUMBE WENZAKE. NA AKAKABIDHISHA MAMBO MEMA (asifanye) TUTAMSAHILISHIA  NJIA YA KUENDEA MOTONI. NA MALI YAKE HAYATAMFAA ATAKAPOKUWA ANADIDIMIA (motoni humo).” (92:8-11)

Mtu anapojifanyia ubakhili yeye mwenyewe, akajidai na kujidhiki na il-hali ameneemeshwa na Mola wake kwa neema ya mali.

Tena akaizuia na akaacha kuitumia katika njia za kheri kwa manufaa yake na ya jamii yake.

 Kazi yake ikawa ni kuchuma na kulimbikiza tu, huyu ni mtu mbaya achukiwaye machoni mwa jamii, asiyependeza mbele yao bali mbele ya mwenye mali yake (Allah)

Huyu hana njia ya kuikwepa adhabu ya Allah iliyotajwa ndani ya aya hii:

(…..NA WALE WAKUSANYAO DHAHABU NA FEDHA WALA HAWAZITOI KATIKA NJIA YA ALLAH, WAPE HABARI ZA ADHABU INAYOUMIZA. (inayowangoja). SIKU (mali yao) YATAKAPOTIWA MOTO KATIKA MOTO WA JAHANAMU, NA KWA  HAYO VINACHOMWA VIPAJI VYA NYUSO ZAO NA MBAVU ZAO NA MIGONGO YAO, (na huku  wanaambiwa) HAYA NDIYO (yale mali) MLIOJILIMBIKIZIA (mliojikusanyia) NAFSI ZENU, BASI ONJENI (adhabu ya) YALE MLIYOKUWA MIKIKUSANYA (9:34-35).

Kadhalika mtu akiikanusha na kuifukuza neema ya mali aliyopewa na Mola Muumba wake, tena bila ya kujaza fomu ya maombi kwa kufanya  ubadhilifu, ufisadi katika ardhi na kuwadhuru wenziwe.

Huyu pia adhabu kali inamngojea kwa mbele ya Allah:

(NA  (kumbukeni) ALIPOTANGAZA MOLA WENU (kuwa): “KAMA MKISHUKURU, NITAKUZIDISHIENI, NA KAMA MKIKUFURU (jueni) KUWA ADHABU YANGU NI KALI SANA ( 14:7).

Ni vema tukatambua na kuelewa kwamba Allah alipomuumba mwanadamu na akamuumbia mali za ardhini na baharini na kamjaza huba ya mali.

Hakumuacha hivi hivi tu, achume mali kwa namna aitakayo, aibe, anyang’anye, adhulumu, ale rushwa ili mradi tu apate mali na kuipiga teke  dhiki.

Akishaipata aitumie atakavyo, alewe, azini, awakandamize wanyonge na……….na……. Ikiwa yuko anayeitakidi hivyo basi ajue anajidanganya mwenyewe.

Iwapo Mjapani mwanadamu mwenzetu, anatugengeneza gari na kutuwekea  muongozo wa kulitumia na tukienda kinyume na muongozo huo, bila shaka litaharibika na halitofanya kazi kama lilivyokusudiwa na mtengenezaji.

Sasa ni vipi basi, Allah amuumbe mwanadamu, ampe na mali, kisha akamuacha hivi hivi bila ya kumpa muongozo wa namna uya kuichuma na kuitumia.

Hili ni muhali kwa Allah kwa sababu linampa sifa ya upungufu. Rejea muongozo wa namna ya kuitumia mali katika aya zilizofungua somo letu hili.    

MALI NA NAMNA YA KUITUMIA

Hii pia ni miongoni mwa tabia njema ambazo muislamu anapaswa kujijpamba nazo kuhusiana na hili tunasoma:

NA UMPE JAMAA (YAKO) HAKI YAKE NA MASIKINI NA MSAFIRI ALIYEHARIBIKIWA, WALA USITAWANYE (mali yako) KWA UBADHIRIFU.” [17 : 26]

 Tuzidi kusoma kwa kutafakari:

“WALA USIFANYE MKONO WAKO (kama) ULIOFUNGWA SHINGONI MWAKO, WALA USIUKUNJUE OVYO OVYO, UTAKUWA NI MWENYE KULAUMIWA (ukifanya hivyo) NA KUFILISIKA (ukiukunjua ovyo ovyo). “[17:29]

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *