SWALA YA MGONJWA

Swala ndio nguzo ya pili miongoni mwa nguzo tano za Uislamu.

Kwa hivyo basi kuihifadhi swala kwa kuiswali namna itakiwavyo na kwa wakati uliowekwa na sheria ni kielelezo kinachoonyesha nguvu ya imani ya mja.

Kama ambavyo ni nembo ya ukweli wa Uislamu wa mja huyo na ni ishara ya mafungamano na mawasiliano yasiyokatika ya kila siku baina ya mja na Allah Mola Muumba wake.

Uislamu kama mfumo sahihi wa maisha ni dini ya maumbile inayoyatambua fika maumbile ya waumini wake na wanadamu kwa ujumla.

Uislamu unatambua kwamba muislamu/mwanadamu hupitia vipindi mbalimbali vya mpito, sambamba na mabadiliko ya kimaumbile kulingana na hatua za uhai anazozipitia.

Miongoni mwa vipindi vya mpito anavyovipitia mwanadamu ni uzima (siha) na ugonjwa na hivi ni vitu/mambo yaliyo nje ya uweza wake.

Kwa kuizingatia hali na mazingira haya anayoyapitia mwanadamu na ili mgonjwa asikatikiwe na mawasiliano na Mola wake, Uislamu umemuwekea utaratibu maalumu wa kuitekeleza ibada hii mama (swala).

Uislamu ukakariri na kutangaza kwamba ye yote miongoni mwa waislamu waliopasiwa na swala atakayekuwa mgonjwa.

Mgonjwa huyu akawa hawezi kuswali swala tano za fardhi kwa kusimama. Kusimama wima ambako ni miongoni mwa nguzo za swala ambazo swala haisihi ila kwa kuzitekeleza zote ipasavyo.

Huyu anaruhusiwa kuiswali swala hiyo ya fardhi kwa KUKAA KITAKO, na kama hawezi kuswali kwa kukaa ataswali kwa kulala ubavu na kuotezea (kuashiria) rukuu na sijida.

Ili kutofautisha baina ya nguzo mbili hizi; rukuu na sijida, anatakiwa kuotezea zaidi katika sijida kuliko rukuu. Tuitegee sikio la usikivu Qur-ani Tukufu:

“AMBAO HUMKUMBUKA ALLAH WAKIWA WIMA NA WAKIKAA NA WAKILALA…” [3:191]

Imekuja riwaya kutoka kwa Imraan Ibn Huswayn-Allah amuwiye radhi-amesema: Nilipatwa na maradhi ya bawasiri (Hemorrhoids), nikamuuliza Mtume-Rehema na Amani zimshukie-kuhusiana na swala (niswali vipi), akanijibu:

“Swali kwa kusimama, ikiwa huwezi basi (swali) kwa kukaa na iwapo huwezi basi (swali) kwa kulalia ubavu wako”. Bukhaariy

Linalozingatiwa (kipimo) katika kutokuweza au kushindwa kusimama au kukaa ni ugumu, uzito au shida inayoweza kumpata mgonjwa kutokana na ama kusimama au kukaa.

Pia kushindwa huzingatiwa kwa ama kuzidi maradhi au kuchelewa kupona iwapo atakaa au kusimama.

Tumia vipimo hivi katika kupimia mambo mengine ambayo yanayoweza kupelekea kuzidi maradhi au kuchelewa kupona au kumtia mtu machungu.

Namna ya mkao ambao unakuwa badali ya kusimama ni mkao wa ‘Tarabui’-(cross legged), yaani mkao wa kukalia tako na kupitisha mguu chini ya mwingine mithili ya herufi “X”.

Hivi ndivyo ilivyopokelewa kutoka kwa mama wa waumini (mkewe Mtume); Bi. Aysha-Allah amuwiye radhi-amesema:

“Nilimuona Mtume-Rehema na Amani zimshukie-akiswali kwa kukaa mkao wa Tarabui”. Nasaai

Pia kunajuzu kukaa mkao wa tashahudi au mkao mwingine wo wote auwezao, hivi ni iwapo hawezi mikao hii tuliyoitaja.

Ama namna ya kuswali kwa mtu ambaye aliyeshindwa kusimama na kukaa, huyu anapewa ruhusa ya kuswali kwa kulala ubavu kama tulivyotangulia kueleza.

Akitoweza hivyo, basi na aswali kwa kulala chali (kimangalimangali) ilhali miguu yake ameilekezea Qiblah kwa kiasi cha uweza wake.

Amesema Sheikh Abdurahmaan AL-jazaairiy-Allah amrehemu-katika kitabu chake kiitwacho (AL-FIQ-HU ‘ALAL-MADHAAHIBIL-‘ARBAA) juzuu ya kwanza:

“Na kama mgonjwa hawezi kufanya cho chote miongoni mwa matendo ya swala ila kwa kuashiria (kitendo) hicho kwa macho yake. Au kuyapitisha matendo hayo moyoni mwake, kutamuwajibikia kuswali hivyo awezavyo na wala swala haimpomokei (haimuondokei) maadam ana akili timamu”.

 

SWALA YA MGONJWA

Swala ndio nguzo ya pili miongoni mwa nguzo tano za Uislamu.

Kwa hivyo basi kuihifadhi swala kwa kuiswali namna itakiwavyo na kwa wakati uliowekwa na sheria ni kielelezo kinachoonyesha nguvu ya imani ya mja.

Kama ambavyo ni nembo ya ukweli wa Uislamu wa mja huyo na ni ishara ya mafungamano na mawasiliano yasiyokatika ya kila siku baina ya mja na Allah Mola Muumba wake.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *