Sharti tunazozikusudia hapa ni zile sharti za kusihi swala.
Maana ya sharti :-
Sharti ya kitu ni lile jambo au tendo ambalo upatikanaji wa kitu husika unalitegemea jambo/tendo hilo lakini lenyewe si sehemu ya kitu hicho.
Mfano : wa ufafanuzi
Mmea ili upatikane/uwepo juu ya uso wa ardhi unahitaji mvua pamoja na ukweli kwamba mvua sio sehemu ya mmea huo.
Kwa hivyo basi mvua ni sharti katika upatikanaji na kuwepo kwa mmea kwani bila ya mvua hakuna mmea lakini bado mvua haiwi ni sehemu ya mmea huo.
Baada ya kujua ainisho la sharti, hebu sasa tuziangalie sharti za kusihi kwa swala moja baada ya jingine kwa ufafanuzi wa kina sharti za kusihi swala ni nne zifuatazo:-
It’s very good