KUWA BAINA YA KHOFU NA MATUMAINI

Ndugu mpenzi katika imani-Allah atuwafikishe kupendana kwa ajili yake-ni wajibu wetu kumuhimidi Allah aliyetuwafikisha  kuusiana mema na kukatazana mabaya.

Ni kheri kwetu ikiwa tutafahamu kwamba miongoni mwa mambo yenye kuokoa ni mja kuwa katika hali ya baina ya khofu na matumaini.

Kuwa katika hali baina ya khofu na matumaini ni katika jumla ya daraja tukufu zinazopasa kuwaniwa na kila muislamu. Allah Mola Mtukufu amewasifia mitume wake na wafuasi wao wema kwa sifa mbili hizi pale aliposema:

WANATUMAI REHEMA ZAKE NA WANAOGOPA ADHABU YAKE. HAKIKA ADHABU YA MOLA WAKO NI YA KUOGOPWA”. [17:57]

Allah akasema tena:

“…BILA SHAKA WAO WALIKUWA WEPESI WA KUFANYA WEMA, NA WAKITUOMBA KWA SHAUKU (ya kupata pepo) NA KHOFU (ya moto). NAO WALIKUWA WAKITUNYENYEKEA”. [21:90]   Allah anazidi kutuambia: “HAKIKA WALE WALIOAMINI NA WALE WALIOHAJIRI (wakahama kuja Madinah) NA WAKAPIGANIA NJIA YA ALLAH, HAO NDIO WANAOTUMAI REHEMA YA ALLAH. NA ALLAH NI MWINGI WA KUSAMEHE (na) MWINGI WA KUREHEMU”. [2:218]

Allah akasema tena:

“NA HAO AMBAO WANATOA (zaka na sadaka katika mali) WALIYOPEWA, NA HALI NYOYO ZAO ZINAOGOPA KWA KUWA WATAREJEA KWA MOLA WAO”. [23:60]

Bibi Aysha (mama wa waumini)-Allah amuwiye radhi-alisema:

Ewe Mtume wa Allah [HAO AMBAO WANATOA (zaka na sadaka katika mali) WALIYOPEWA NA HALI NYOYO ZAO ZINAOGOPA] ni yule ambaye anayeiba, anazini na anakunywa pombe na ilhali anamuogopa Allah Mtukufu? (

Mtume) akasema:

“Hapana ewe Bint ya Abu Bakri, ewe Bint Swidiq, lakini huyo (akusudiwaye na aya) ni yule ambaye anayeswali, akafunga na akatoa sadaka na ilhali anamuogopa Allah Mtukufu”. Ahmad, Tirmidhiy & Ibn Abiy Haatim-Allah awarehemu.

Fahamu na ujue ewe ndugu yangu kwamba khofu ni kikatazi na kikemezi kinachomkataza mwanadamu na kumkemea na maasi.

Na matumaini ni kiongozi anayeshika hatamu za kumuongoza mja kuelekea katika mambo ya twaa.

Kwa mantiki hii basi, mtu ambaye khofu yake haimkatazi maasi na wala matumaini yake hayamuongozei katika twaa.

Khofu na matumaini yake haya ni hadithi ya moyo isiyopewa uzito wala mazingatio.

Kutokupewa uzito huko na kule kutokuzingatiwa kunatokana na khofu na matumaini hayo kukosa matunda yaliyokusudiwa na faida itakiwayo.

Baadhi ya watu wamekuwa na fahamu lemavu kuelekea maana/dhana ya kuwa na matumaini kwa Allah.

Wakadhania kwamba maana yake ni kuhalalisha kutenda maasi na kuendelea nayo kwa kutegemea ukunjufu wa rehema za Allah.

Hawa wakaangamia na wataangamia bila ya kukusudia.

Wengi miongoni mwa watu wa tabaka la kawaida wametumbukia katika utumwa wa fikra lemavu hizi, wakaghurika.

Matuamini yaliyo chini ya mwavuli huu mbovu, haya ni matumaini ya uongo nako ni kudanganyika na kujidanganya na si vinginevyo.

Wala haya sio yale matumaini mema anayopaswa kuwa nayo kila muumini. Matumaini mema ni yale yanayomuongoza mja kumtii Mola Muumba wake katika yote; maamrisho na makatazo yake na kumpitisha njia airidhiayo Allah.

Ewe ndugu yangu-Allah akuhidi-tahadhari kufanya maasi huku ukitarajia kufunikwa na rehema za Mola wako, hiyo ni ghururi akupandikiziayo shetani mlaaniwa na ni shari aliyokuletea katika sura na umbo la kheri.

Kisha tahadhari tena tahadhari kweli kujiaminisha na adhabu ya Allah na kukata tamaa na rehema zake. Hebu na tuizingatie kwa pamoja kauli tukufu ya Allah Mola Mtukufu:

 “JE, WAMEAMINISHA KUADHIBIWA NA ALLAH? HAWAAMINISHI ADHABU YA ALLAH ILA WATU AMBAO (watakuwa) WENYE KHASARA”. [7:99]

Al-Hassan Al-Biswriy-Allah amrehemu-amesema:

“Muumini hufanya mambo ya twaa na ilhali ana khofu na uoga (na adhabu ya Allah). Na faajiri (mtu muovu) hufanya maasi ilhali akijiaminisha (na adhabu ya Allah)”.

Allah akasema tena:

“AKASEMA: NA NANI ANAYEKATA TAMAA YA REHEMA YA MOLA WAKE ISIPOKUWA WALE WALIOPOTEA?” [15:56]

Pengine ndugu yangu utataka kuniuliza nini maana ya kujiaminisha na adhabu ya Allah na kukata tamaa na rehema ya Allah.

Ikiwa hivyo ndivyo, haya naomba unitegee sikio lako nikujuze. Tunaposema kujiaminisha na adhabu ya Allah tunakusudia kuwa na matumaini matupu yasiyoshehenezwa na amali njema.

Na kutokuwa na khofu ya Allah kabisa kiasi cha kuamini kwamba hakujuzu kwa Allah kumuadhibu kwa hayo maovu ayatendayo.

Ama kukata tamaa na rehema ya Allah ni kuwa na khofu tupu isiyosuhubiana na amali njema. Na kutokuwa na matumaini kwa Allah kiasi cha kuamini kwamba hakujuzu kwa Allah kumrehemu na kumsamehe. Hiyo ndiyo maana sahali ya ibara mbili hizo, elewa ufahamu.

Kujiaminisha na adhabu ya Allah na kukata tamaa na rehema yake ni miongoni mwa madhambi makubwa, tahadhari na mawili haya ewe ndugu yangu uiokoe nafsi yako na hilaki.

Kuwa baina ya khofu na matumaini na usighurike kwa Mola wako na wala usijijasirishe mbele yake kwani:

“…HAKIKA MOLA WAKO NI MWEPESI WA KUADHIBU NA HAKIKA YEYE NI MWINGI WA KUSAMEHE (na) MWINGI WA KUREHEMU (kwa wale wanaorejea kwake)”. [6:165]

Mpenzi ndugu yangu-Allah atusitiri-hebu na tukamilishe huku kuusiana kwetu mema na kukatazana maovu, kwa kuzizingatia kauli hizi za Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie:-

      “Lau muumini angelijua adhabu iliyoko kwa Allah asingeliitumai pepo yake ye yote. Na lau kafiri angeliijua rehema iliyoko kwa Allah asingekata tamaa ya pepo ye yote”. Ahmad-Allah amrehemu.

    “Allah ameumba rehema mia moja, akaiweka rehema moja (tu) baina ya viumbe wake warehemeane kwayo. Na tisini na tisa (zilizobaki) ziko kwa Allah”. Tirmidhiy-Allah amrehemu.

KUWA BAINA YA KHOFU NA MATUMAINI

Ndugu mpenzi katika imani-Allah atuwafikishe kupendana kwa ajili yake-ni wajibu wetu kumuhimidi Allah aliyetuwafikisha  kuusiana mema na kukatazana mabaya.

Ni kheri kwetu ikiwa tutafahamu kwamba miongoni mwa mambo yenye kuokoa ni mja kuwa katika hali ya baina ya khofu na matumaini.

Kuwa katika hali baina ya khofu na matumaini ni katika jumla ya daraja tukufu zinazopasa kuwaniwa na kila muislamu. Allah Mola Mtukufu amewasifia mitume wake na wafuasi wao wema kwa sifa mbili hizi pale aliposema:

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *