NYUDHURU ZA KUACHA SWALA YA JAMAA NA IJUMAA

Nyudhuru zinazoweza kumfanya mtu kutokuhudhuria swala ya jamaa msikitini, zinagawika katika mafungu mawili makuu kama ifuatavyo:-

a) NYUDHURU JUMUIA:

Hizi ni pamoja na mvua kubwa, upepo mkali wakati wa usiku na matope mengi njiani  kiasi cha kumchafua mtu au kumuangusha.

Imepokelewa kwamba Ibn Umar-Allah awawiye radhi–aliadhini kwa ajili ya swala katika usiku wenye baridi na upepo mkali, kisha akasema:

ALAA SWALUU FIR-RIHAAL Maana yake:

“Ehee swalini majumbani mwenu”. Kisha akasema: Hakika Mtume wa Allah–Rehema na Amani zimshukie–alikuwa akimuamuru muadhini, uwapo usiku wenye baridi na mvua kusema:

ALAA SWALLUU FIR-RIHAAL. Bukhaariy & Muslim Leo kutokana na maendeleo ya miji si rahisi kupatikana nyudhuru hizi mijini ambamo nyumba zimeungana, barabara zina lami na mataa yanawaka pia watu wana makoti ya mvua na miavuli. Kwa hivyo utaona kama kwamba nyudhuru hizi hazina nafasi mijini na badala yake zinaweza kutumika zaidi vijijini.

 

b) NYUDHURU BINAFSI:

Hizi ni pamoja na maradhi, njaa au kiu kikali, khofu ya dhalimu kwa nafsi au mali, kubanwa na haja kubwa au ndogo, kuwekwa (kutengwa) chakula na mtu akawa na njaa au anakitamani chakula hicho na kula kitu chenye kunuka (harufu kali) mithili ya kitunguu thaumu.

Amesema Mtume wa Allah–Rehema na Amani zimshukie:

“Kitapowekwa chakula cha usiku (Ashaa) cha mmoja wenu na ikakimiwa swala, basi anzeni na kile chakula na mtu asifanye haraka mpaka amalize kula (ndio aswali)”. Bukhaariy & Muslim

“Hapana swala mbele ya chakula, wala (wakati) yeye kabanwa na machafu mawili (haja kubwa na ndogo)”. Muslim

“Atakayekula kitunguu thaumu, basi na ajitenge nasi”. Au alisema:

“…Na ajitenge na msikiti wetu, na akae (aswali) nyumbani kwake”. Bukhaariy & Muslim

Kila moja miongoni mwa hali hizi tulizozitaja hapa zinazingatiwa kuwa ni udhuru wa kisheria unaoweza kumfanya mtu asihudhurie swala ya jamaa.

Nyudhuru hizi zote kama zinaashiria jambo, basi jambo hilo halitakuwa ila ni wema na wepesi wa dini hii ya maumbile:

“…ALLAH ANAKUTAKIENI YALIYO MEPESI WALA HAKUTAKIENI YALIYO MAZITO…”  (2:185)

 

 SHARTI ZA IMAMU.

Swala ya jamaa huwakusanya pamoja Imamu mmoja na maamuma mmoja au zaidi ya mmoja.  Imamu ndio kiongozi katika ibada hii ya swala na maamuma wote walioko nyuma yake wanalazimishwa kumfuata. 

Kwa hivyo basi Imamu anachukua dhima kuu mbele ya waja na mbele ya Allah, kutokana na uzito wa dhima hii, imeshurutizwa Imamu awe na sifa zifuatazo:-

  1. Mwanamume: Hausihi uimamu wa mwanamke kuwaswalisha wanamume ila kwa wanawake wenzake.
  2. Muadilifu: Hafai kuwa Imamu mtu fasiki wenye kujulikana ufasiki wake ila atapokuwa sultani (kiongozi) mwenye kuchelewa shari yake.
  3. Mjuzi: Awe na elimu ihusianayo na swala, tangu twahara na swala yenyewe pamoja na vipengele vyake vyote.  Haisihi kuwa Imamu mjinga asiye na elimu ila kwa watu mfano wake (wajinga wenziwe).
  4. Mkubwa: Imamu asiwe mwana mdogo ambaye hajafikia baleghe, kwa sababu yeye si katika watu wenye taklifu.
  5. Akili: Mwendawazimu hafai kuwa Imamu, kwa sababu siyo mukalafu kisheria.

 

MWENYE HAKI YA KUWA IMAMU.

     Mwenye haki ya kuwa Imamu miongoni mwa watu ni:-

  1. Msomi wao zaidi wa kitabu cha Allah, yaani aliyehifadhi Qur-ani na kuisoma vizuri itakiwavyo kwa mujibu alivyofundisha Mtume wa Allah.
  2. Kisha mwenye kuijua vema dini ya Allah, yaani anajua sheria khususan hukumu za swala na mambo yote yenye kufungamana nayo.
  3. Kisha mwenye wingi wa taq-wa, yaani matendo yake ya dhahiri yanaonyesha kuwa ni mcha–Mungu.
  4. Kisha mwenye umri mkubwa kuliko wote.

Huu ndio utaratibu kama alivyoupanga mwenyewe Bwana Mtume– Rehema na Amani  zimshukie–katika kauli yake: “Awaswalishe watu (awe Imamu wao) msomi wao wote wa kitabu cha Allah, wakilingana sawa katika huo usomaji (wa kitabu cha Allah) basi (awe imamu) mjuzi wao wa suna (ya Mtume). Wakilingana sawa katika kuijua suna, basi (awe imamu) mtangulizi wao kwa Hijrah. Na wakilingana sawa katika Hijra basi (awe imamu) mkubwa wao kwa umri”. Muslim

 

TANBIHI:

Akiwepo kiongozi, basi yeye ndiye mwenye haki zaidi ya kutawalia uimamu katika mamlaka yake. Haimfalii mtu mwingine ye yote kumtangulia ila kwa idhini yake.

Kadhalika atapokuwepo Imamu aliyechaguliwa na watu wa sehemu husika na kupewa jukumu na watu wa sehemu hiyo na kupewa jukumu hilo la uimamu.

Haisihi mtu mwingine kumtangulia imamu huyu ila kwa idhini yake.  Pia haifai mtu mwingine kumtangulia mwenye nyumba nyumbani kwake ila kwa idhini yake.

Haya ndiyo mafunzo yatokanayo na kauli ya Mtume wa Allah– Rehema na Amani zimshukie: “Mtu asiwe asiwe imamu wa mtu kwa watu wake (nyumbani kwake) wala katika mamlaka yake ila kwa idhini yake”.

 

MAS–ALA.

   Ni vema mtu kuyajua mas-ala haya katika suala zima la uimamu:-

  1. UIMAMU WA MWANAMKE:

Inasihi mwanamke kuwa Imamu akawaswalisha wanawake wenzake. Kiutaratibu yeye hasimami mbele yao kama asimamavyo Imamu mwanamume, bali yeye atasimama katikati yao katika safu. 

Hili linatokana na idhini ya Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie– aliyompa Ummu Waraqah Bint Naufal.  Idhini ya kujiwekea muadhini wake nyumbani mwake, aadhini kisha yeye (Ummu Waraqah) apate kuwaswalisha watu wake wa nyumbani. 

Haya ni kwa mujibu wa riwaya iliyopokelewa na Imamu Abuu Daawoud.

 

  1. UIMAMU WA KIPOFU:

Inasihi kipofu kuwa imamu kwa sababu Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie-alimpa Ibn Ummu Maktuum ukhalifa wa Madinah mara mbili. Nae–Allah amuwiye radhi–akawa anawaswalisha watu na     ilhali yeye ni kipofu. Hivi ndivyo inavyoeleza riwaya ya Abuu Daawoud.

 

  1. UIMAMU WA ALIYE CHINI KATIKA DARAJA YA UIMAMU:

Inasihi kuwa imamu mtu aliye chini katika daraja ya uimamu pamoja na kuwepo aliye bora kuliko yeye.

Hili linatokana na kitendo cha Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie–kuswali nyuma ya Sayyidna Abuu Bakri na nyuma ya Abdur-rahmaan Ibn Auf na il-hali yeye Bwana Mtume ni bora kuliko wao bali kuliko viumbe wote.  Hivyo ndivyo ilivyokuja katika riwaya ya Imamu Bukhaariy.

 

  1. UIMAMU WA MTU ALIYETAYAMAMU:

Inasihi mtu aliyetayamamu kumswalisha mtu aliyetawadha.  Hii ni kwa sababu Amrou Ibn Al-Aaswi alikiswalisha kipote (kikundi) cha vita (sariyah) nae akiwa ametayamamu na maamuma wake wakiwa wametawadha.

Khabari hii ikamfikia Bwana Mtume nae hakukanusha wala kulikemea hilo na hivyo kufahamika kuwa amelikiri.  Hivi ndivyo ilivyo katika riwaya ya Abuu Daawoud.

 

  1. UIMAMU WA MSAFIRI:

Inasihi msafiri kuwa imamu wa mkazi (asiye msafiri) isipokuwa itamlazimu huyu mkazi kuitimiza swala yake baada ya imamu wake msafiri kutoa salamu. 

Hili linatokana na kitendo cha Mtume wa Allah– Rehema na Amani zimshukie–kuwaswalisha watu wa Makah nae akiwa msafiri, na akawaambia:

“Enyi watu wa Makah, timizeni swala zenu kwani sisi ni wasafiri”. Imam Maalik

Na kama msafiri ataswali nyuma ya mkazi, atatimiza pamoja nae.  Aliulizwa Ibn Abasi–Allah awawiye radhi–kuhusiana na suala la kutimiza msafiri nyuma ya mkazi, akasema:

“Hiyo ni sunah ya Abul-Qaasim (Mtume)”.  Ahmad

 

NYUDHURU ZA KUACHA SWALA YA JAMAA NA IJUMAA

Nyudhuru zinazoweza kumfanya mtu kutokuhudhuria swala ya jamaa msikitini, zinagawika katika mafungu mawili makuu kama ifuatavyo:-

a) NYUDHURU JUMUIA:

Hizi ni pamoja na mvua kubwa, upepo mkali wakati wa usiku na matope mengi njiani  kiasi cha kumchafua mtu au kumuangusha.

Imepokelewa kwamba Ibn Umar-Allah awawiye radhi–aliadhini kwa ajili ya swala katika usiku wenye baridi na upepo mkali, kisha akasema:

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *