UPOLE

Upole ni dhana ambayo huweza kutofautiana baina ya mtu na mtu, jamii na jamii nyingine, dini na dini kulingana na mtazamo wa mtu/jamii au dini husika juu ya dhana nzima ya upole.

 Tunamaanisha na kukusudia nini tunapozungumza dhana ya upole?

Makala haya yamekusudia kuiangalia na kuieleza dhana hii ya upole chini ya kivuli cha uislamu kupitia Qur-ani Tukufu na Sunnah ya Bwana Mtume –Rehema na Amani zimshuke.

Tusome kwa mazingatio:-

“KWA YAKINI IBRAHIMU ALIKUWA MPOLE MWENYE KUMTUKUZA ALLAH NA MWEPESI WA KUREJEA (kwake)”.[11:75]

Qur-ani Tukufu inatufahamisha kupitia aya hiyo hapo juu kwamba:-

  1. Kumbe upole ni sifa njema waliyopambika nayo mitume wa mwenyezi mungu japokuwa hapa ametajwa Nabii Ibrahimu- Rehema na Amani ziwashukie wote.

 

  1. Upole ni sifa muhimu ya kiutendaji ambayo Mjumbe/Mtume/Mtumishi yeyote wa ummah hana budi kuwa nayo ili imsogeze karibu na watu wake. Huku kuwa karibu na watu wake kutamrahisishia mawasiliano yake nao jambo ambalo litamwepesishia kazi yake.

 

  1. Pole wa kweli na halisi ni ule uambatanao na sifa mbili muhimu ambazo ni :-
    1. Kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu.
    2. Wepesi wa kurejea kwa Mwenyezi Mungu kuomba msamaha mara tu kosa litendekapo.

Kupitia aya hii tunaweza sasa tukaieleza dhana ya upole kuwa ni kudhibiti nafsi wakati wa mafuriko ya ghazabu au kuacha kulipa kisasi dhidi ya adui/mbaya wakati wa kuweza kulitekeleza hilo na kuendelea kuwa karibu na mtu huyo.

Kuna mambo kadhaa ambayo kwa kiasi kikubwa kuchangia kumfanya mtu awe na sifa hii njema na tukufu ya upole ambayo inatakiwa iwe ni pambo na vazi la kila muislamu.

Tukubaliane na tuyaite mambo hayo kuwa sababu/msingi ya upole. Miongoni mwa sababu hizo ni:-

  1. Kuwa na huruma. :

Ni muhali kabisa mtu kuwa mpole ikiwa hamna ndani ya moyo wake chembe ya huruma, kwani ni hisia za huruma ndizo ambazo humfanya mtu kuwa mpole kiasa cha kuacha kumuangamiza mbaya wake il-hali ana uwezo na nguvu za kulitekeleza hilo. Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie- anutuambia :- “Asiyehurumia (hastahiki)kuonewa huruma.”

  1. Kujiepusha na kuwashutumu na kuwatukana watu.

Kitendo cha kushutumiana na kutukanana hupeleka kujenga chuki na moyo wa kulipiza kisasi baina ya watu.

Ni bayana kwamba palipotawaliwa na chuki na visasi hapana huruma na pasipo na huruma hapana upole.

Hii ndio sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu akatukataza kuwatukana washirikina/makafiri ili tusisababishe kutukanwa Mwenyezi Mwenyezi Mungu, jambo ambalo waumini wa kweli hawatalivumilia na watataka kuliondosha kwa nguvu zao zote hapo ndipo hasira, chuki na visasi vitatawala pande zote mbili na kuzifukuzilia mbali huruma na upole na kusababisha umwagikaji wa damu usio wa lazima. Tusome na tuzingatie:-

“WALA MSIWATUKANE WALE AMBAO WANAABUDU KINYUME CHA ALLAH, WASIJE WAKAMTUKANA ALLAH KWA JEURI ZAO BILA KUJUA….[6:108]

  1. Kuwa na haya

Kuwa na haya ni kuhifadhi na kuichunga nafsi na kila ambalo kwa namna moja ama nyingine linaweza kuwa ni sababu ya kuvunja heshima na hadhi ya mtu mbele ya jamii.

 Pia kuwa na haya huonyesha kukamilika kwa murua wa mtu.

Mtu anapojivika joho la haya, haya itamsukuma kujichunga sana katika utendaji wake katika kuchanganyika kimaisha na wenziwe.

Hatofanya la kuwaudhi au kuwakera wenziwe ili naye asije kufanyiwa, hatakuwa ni chanzo/sababu ya kuvunja heshima ya wengine ili kuhifadhi heshima yake isivunjwe.

 Huyu atakuwa akiuzingatia na kuishi na msingi wa busara usemao: “utendavyo ndivyo utakavyotendewa”.

Mtu anapokosa haya, huwa hana huruma na hivyo kutokuchunga wala kujali heshima na hadhi za watu wengine. Ni kutokana na umuhimu na nafasi ya sifa hii inayompamba na kumfanya mtu kuwa mpole ndio Bwana Mtume –Rehema na Amani zimshukie akatuambia : “haya ni sehemu ya imani….”Ahmad.

  1. Kuacha kuzungumza maneno ya ufedhuli ya upuzi yasiyo na maana

Katika kusema maneno ya ufadhuli kutapelekea kuhimiza hisia za watu na pengine kuzusha hali ya kutokuelewana na kusababisha kuvunjika kwa amani baina ya pande mbili husika.

Ni kwa kulizingatia hilo ndipo Bwana Mtume-Rehema na amni zimshukie-akatuasa :-

“Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, basi na aseme la kheri {ikiwa hana}na anyamaze

Kwa mantiki hii kuacha kwako kusema maneno ya ufedhuli huonyesha kuwajali kwako wenzio, na hili haliji hivi hivi tu bali husababishwa na huruma iliyomo ndani ya nafsi ambayo humfinyanga mtu kuwa mpole.

Mambo haya ni baadhi tu ya msingi, sababu na vyanzo vya sifa njema ya upole ambayo ni rasilimali kubwa ya mtu.

Tujipambe na sifa hii ili nasi tuipate daraja kubwa iliyoandaliwa maalumu kwa ajili ya watu wapole tuisome na kuuamini kauli ya Bwana Mtume –Rehema na Amani zimshukie:-

 “Hakika mtu huridhika/ hupata kwa sababu ya upole daraja ya mfungaji {mchana} asimamaye{usiku kufanya ibada}” 

 

UPOLE

Upole ni dhana ambayo huweza kutofautiana baina ya mtu na mtu, jamii na jamii nyingine, dini na dini kulingana na mtazamo wa mtu/jamii au dini husika juu ya dhana nzima ya upole.

 Tunamaanisha na kukusudia nini tunapozungumza dhana ya upole?

Makala haya yamekusudia kuiangalia na kuieleza dhana hii ya upole chini ya kivuli cha uislamu kupitia Qur-ani Tukufu na Sunnah ya Bwana Mtume –Rehema na Amani zimshuke.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *