SAFARI YA MTUME NA AMMI YAKE KUELEKEA SHAMU

Bwana Mtume –Allah amshushie rehema na amani- alipofikia umri wa miaka kumi na nane alisafiri pamoja na ammi yake Abu Twalib kuelekea Shamu.

Hii ilikuwa ni safari ya kibiashara. Walipofika katika HUURAANA wakiwa njiani kuelekea BASRAH nchini Shamu, hapo padri wa kiyahudi jina lake Bahiyrah alimuona Mtume akifunikwa na kiwingu kutokana na jua kali la jangwani wakati msafara wao ulipokuwa unakaribia hapo.

Msafara ukaja ukapumzika chini ya mti uliokuwa jirani na kibanda cha padri yule, padri akakiona kiwingu kimefunika mti ule waliopumzika chini yake Mtume na watu wengine waliokuwemo katika msafara ule wa kibiashara, akayaona matawi ya mti ule yamemuinamia kijana mmoja aliyekuwemo katika msafara ule.

Bahiyrah alikuwa mwanachuoni wa kiyahudi na alikuwa amesoma katika TAURATI na INJILI juu ya Mtume atakayetokea Bara Arabu.

Bahiyrah akaandaa chakula na kuualika msafara mzima katika karamu nyumbani kwake kinyume na ada yake, kwani hakuwa na tabia ya kuwaalika chakula watu nyumbani kwake.

Msafara ulipohudhuria karamu, Bahiyrah akawa anamkazia sana macho Bwana Mtume na akiziangalia alama alizokuwa nazo Mtume mwilini mpaka akafanikiwa kuuona muhuri wa utume ulokuwa baina ya mabega yake.

Hapo ndipo padri Bahiyrah akamuuliza Bwana Mtume juu ya hali na mambo yanayomtokea akiwa yu macho au usingizini.

Bwana Mtume akamueleza yote yanayomtokea bila ya kuficha hata jambo moja, Bahiyrah akaona aliyoelezwa na Mtume ndio sifa za Mtume aliyebashiriwa katika kitabu alichonacho yeye yaani Taurati.

Bahiyrah akatambua kijana huyu ndiye Mtume angojewaye, ndipo akauliza wageni wake waalikwa khabari za kijana yule na amefuatana na nani katika msafara ule. Wakamuelekeza kwa ammi yake Bwana Abuu Twalib akamwambia :

“Mrejeshe mwanao huyu Makkah usiende naye Shamu kwani mayahudi watakapomuona na kumtambua ndiye Mtume angojewaye watamuua kutokana na chuki ya kuhama utume kwao na kwenda kwa waarabu.” Abuu Twalib akazisikiliza nasaha za Bahiyrah na akarudi naye haraka Makkah

SAFARI YA MTUME NA AMMI YAKE KUELEKEA SHAMU

Bwana Mtume –Allah amshushie rehema na amani- alipofikia umri wa miaka kumi na nane alisafiri pamoja na ammi yake Abu Twalib kuelekea Shamu.

Hii ilikuwa ni safari ya kibiashara. Walipofika katika HUURAANA wakiwa njiani kuelekea BASRAH nchini Shamu, hapo padri wa kiyahudi jina lake Bahiyrah alimuona Mtume akifunikwa na kiwingu kutokana na jua kali la jangwani wakati msafara wao ulipokuwa unakaribia hapo.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *