HIJRA YA KWANZA YA UHABESHI (ERITREA)

Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie – alipoona kwamba Makurayshi wanazidi kuendeleza sera yao ya mateso na ukatili dhidi ya maswahaba kwa ajili tu ya kulinda hadhi na heshima ya miungu yao na nafasi yao baina ya Waarabu isichukuliwe na Uislamu.

Kadhalika Mtume alipoona kuwa yeye hana ubavu wa kukabiliana na kupambana na Makurayshi ili kuiondosha dhulma hii kwa maswahaba wake na akaiona hatari na fitna inayowanyemelea kutokana na ukali na uchungu wa adhabu na mateso hayo.

Mtume alitambua fika kwamba maswahaba ni wanadamu kama wanadamu wengine, wanaathirika na adhabu na mateso kama watu wengine, adhabu isije ikawafikisha mahala wakajiuliza, hivi ni kwa nini tunaadhibiwa, bila shaka ni kwa ajili ya Uislamu tu, Uislamu ambao unashindwa kututetea na kutuhami, basi ni vema kama tutauacha Uislamu na kurejea katika dini ya mababa zetu ili tusalimike na adhabu na mateso haya tuyapatayo.

Hii ndiyo fitna na hatari aliyoichelea Bwana Mtume kama kiongozi mwenye kuwajibika kwa watu wake alijiona ana wajibu na jukumu la kulitafutia ufumbuzi tatizo hili.

 

Akakaa chini na kutafakari, baada ya kutafakari kwa makini akaona hakuna suluhisho jingine zaidi ya kuwakimbia makurayshi kwa kuhamia Uhabeshi. Akawashauri maswahaba:

“Mnaonaje lau mtatoka mkaelekea Uhabeshi, kwani huko kuna mfalme ambaye mtu hadhulumiwi mbele yake, hiyo ni ardhi (nchi) ya ukweli, mpaka hapo Mwenyezi Mungu atakapokupeni faraja na matokeo kutokana na hali hii (ya adhabu na mateso) mliyo nayo.” Nchi hii ya Uhabeshi ilikuwa ikifuata dini ya unaswara, dini ya Nabii Isa Ibn Mariamu – Rehema na amani zimshuie – Mfalme wa nchi hii Najaash alikuwa ni mfuasi mkweli wa dini hii.

Wakahamia Uhabeshi kutokana na ushauri huu wa Bwana Mtume, wanamume kumi na mbili (12) na wanawake watano (5).

Miongoni mwa wakimbizi na wahamiaji hawa walikuwemo Uthman Ibn Affaan na mkewe Ruqayah binti ya Mtume, Zuberi Ibn al-Awwaam mtoto wa Ami yake bi Khadijah mkewe Bwana Mtume, Uthmaan Ibn Madh-uun, Utbah Ibn Rabia na Mkewe Sahlah Bint suhayl.

Hili ndilo kundi la mwanzo la Waislamu kuhamia Uhabeshi, na hii ndio hijra ya kwanza katika Uislamu. Hijra hii ilikuwa katika mwezi wa Rajab, mwaka wa tano wa utume, yaani tangu Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie – alipokabidhiwa rasmi na Mola wake jukumu la kuuongoza umah.

Waanga na wathirika hawa wa mateso ya makurayshi walipofika Uhabeshi, walipokelewa vema na mfalme Najaash, wakapata tena amani na utulivu walioukosa katika nchi yao wenyewe. Ukarimu, amani na utulivu huu ukawashajiisha kuwatumia ujumbe ndugu zao wengine wanaoadhibiwa Makkah waje kujiunga nao huko.

Hivi ndivyo mfalme huyu muadilifu alivyowatendea wakimbizi hawa waislamu kwa kuyafuata mafundisho sahihi ya Nabii Issa – amani ya Allah imshukie

HIJRA YA KWANZA YA UHABESHI (ERITREA)

Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie – alipoona kwamba Makurayshi wanazidi kuendeleza sera yao ya mateso na ukatili dhidi ya maswahaba kwa ajili tu ya kulinda hadhi na heshima ya miungu yao na nafasi yao baina ya Waarabu isichukuliwe na Uislamu.

Kadhalika Mtume alipoona kuwa yeye hana ubavu wa kukabiliana na kupambana na Makurayshi ili kuiondosha dhulma hii kwa maswahaba wake na akaiona hatari na fitna inayowanyemelea kutokana na ukali na uchungu wa adhabu na mateso hayo.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *