KABILA LA KURAISHI NA UTAWALA WAKE

Makabila mengi yalipatikana kutokana na kizazi cha Ismail mwana wa Nabii Ibrahimu katika nchi ya Hijazi, kabila la Qurayshi ndilo lililokuwa mashuhuri zaidi.

Baadhi ya makabila haya yalikuwa yakimuabudu Mwenyezi Mungu kupitia mafundisho ya dini ya Nabii Ibrahim- Amani ya Allah imshukie.

Uongozi wa kidini na kibiashara ulitawaliwa na Maqurayshi kwa sababu ya ushujaa na ufasaha waliokuwa nao, sifa hizi ndizo zilizolipelekea kabila la Qurayshi kuyatawala makabila mengine yote.

 Mji wa Makkah na Maqurayshi walizidi kupata utukufu pale Mzee Qusway Bin Kilaab-babu wa nne wa Mtume aliposhika hatamu za uongozi wa mji wa Makkah.

Mzee huyu alikuwa ni mtu mwenye busara, fikra na hekima. Alianzisha mpango mji, bunge ili watu wote wa Makkah waweze kukutana humo na kushauriana/kujadili mambo yao, pia aliijenga upya Al-Kaaba baada ya kuanza kuonyesha athari za kubomoka.

 Kadhalika alianzisha utaratibu wa kuwasaidia masikini kwa kuwapa chakula na maji. Baada ya kupita vizazi vingi, taratibu Maqurayshi walianza kuyatupa mafundisho ya dini ya Nabii Ibrahimu na kuanza kuyaabudu masanamu yaliyotengenezwa na mikono yao wenyewe.

Ibada ya msanamu ilikuwa ni matokeo ya safari ya mmoja wa viongozi wa Maqurayshi alipokewenda Shamu na kuwakuta watu wa huko wakiyaabudia masanamu na akapendezwa na kuvutiwa na ibada hiyo.

Akarejea Makkah na sanamu moja, akaliweka ndani ya Al-kaaba na kuanza kuliabudia.

Watu wa Makkah kuona hivyo nao wakamuiga kiongozi wao, wakatengeneza masanamu yao wakayaweka ndani ya Al-kaaba na kuyaabudia na huo ukawa ndio mwanzo wa kuiacha na kuitupa mila ya Nabii Ibrahimu.

KABILA LA KURAISHI NA UTAWALA WAKE

Makabila mengi yalipatikana kutokana na kizazi cha Ismail mwana wa Nabii Ibrahimu katika nchi ya Hijazi, kabila la Qurayshi ndilo lililokuwa mashuhuri zaidi.

Baadhi ya makabila haya yalikuwa yakimuabudu Mwenyezi Mungu kupitia mafundisho ya dini ya Nabii Ibrahim- Amani ya Allah imshukie.

Uongozi wa kidini na kibiashara ulitawaliwa na Maqurayshi kwa sababu ya ushujaa na ufasaha waliokuwa nao, sifa hizi ndizo zilizolipelekea kabila la Qurayshi kuyatawala makabila mengine yote.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *