Kuna aina mbili za josho kwa mtazamo wa kisheria (kifiq-hi):
- Josho la faradhi/wajibu na
- Josho la suna
- JOSHO LA FARADHI :
Hili ni lile josho ambalo haitosihi ibada yenye kuhitajia twahara kama vile swala bila ya kupatikana kwanza josho hili wakati wa kuwepo sababu zake.
SABABU ZA JOSHO LA FARADHI :
Haya ni yale mambo ambayo yakimtokea muislamu yatamsababishia awajibikiwe kukoga josho hili la faradhi. Mambo hayo ni :
- Janaba
- Hedhi/Nifasi
- Kuzaa/Kujifungua
- Mauti (kifo)
Haya ndiyo mambo ambayo humpasia muislamu josho la faradhi yatakapomtokea. Hebu sasa tujaribu kuyafafanua moja baada ya jingine.