AHLUL BAYT WAHAMIA MADINA

 Amesema Ibn Sa’ad – Allah amrehemu:

“Mtume wa Allah alimtuma huru wake Zayd Ibn Haarithah na Abuu Raafii kwenda mjini Makkah kuwahamisha Ahli zake na akawapa ngamia wawili na Dir-ham mia tano (500) ziwasaidie safarini.

(Wakarudi Madinah) na kumletea Fatma na Umuu kulthuum binti za Mtume wa Allah, na Bi. Saudah Bint Zum-ah mkewe (mtume).

Ama Bi Rukia (Bint mwingine wa Mtume) yeye alikwa amekwisha hama zamani pamoja na mumewe: Uthman Ibn Affaan.

Bi Zainab (bint ya Mtume )nae alizuiliwa na mumewe Abul-aaswi Ibn Ar-rabii kuondoka. Zayd Ibn Haarithah akamchukua mkewe, Umuu Ayman pamoja na mwanawe Usaamah.

Abadallah Ibn Abuu Bakri ndiye aliyeondoka na watu hawa pamoja na familia ya Abuu Bakri akiwemo pia Bi. Aysha kuja Madinah.

Akafikia nao katika nyuma ya Bwana haarithah Ibn An-numaan”

Baada ya Ahulu Bayt na Mtume kuhama Madinah wakitokea Makkah ambako usalama wao ulikuwa hatarini. Mtume – Rehema na Amani zimshukie – aliendelea na shughuli yake aliyokuwa ameianza akiwa kama Mtume wa Allah na kiongozi wa mji huo wa madinah.

Aliendelea kuratibu masuala yake na ya jamii ya maswahaba wake ili kuasisi jamii njema itakayopigiwa mfano kwa kila jambo jema.

Jamii itakayojengwa katika misingi ya upendo, udugu, uadilifu, usawa, kusaidiana na kujitoa muhanga kwa jaili ya manufaa ya umma.

Hii ndio misingi na nguzo imara za jamii njema iliyowekwa na mfumo sahihi wa maisha, uislamu ili jamii ya wanadamu mahala popote ilipo na zama zozote iwazo  iweze  kuishi ikiwa kama ndugu moja yenye kusaidiana ikitawaliwa na mshikamano wa kidungu na kufunikwa na wingu la amani na salama.

Hii ndio iliyokuwa sera na siasa aliyoitumia Mtume wa Allah- Rehema na Amani zimshukie ili kuhakikisha kuwa anaasisi jamii njema, yenye utu kamili:

‘NA SHIKAMANANENI KWA KAMBA (dini) YA ALLAH NYOTE, WALA MSIACHANE. NA KUMBUKENI NEEMA YA ALLAH ILIYO JUU YENU., (zamani) MLIKUWA MAADUI, NAYE AKAZIUNGANISHA NYOYO ZENU, HIVYO, KWA NEEMA YAKE, MKAWA NDUGU………………………..(3: 103).

AHLUL BAYT WAHAMIA MADINA

 Amesema Ibn Sa’ad – Allah amrehemu:

“Mtume wa Allah alimtuma huru wake Zayd Ibn Haarithah na Abuu Raafii kwenda mjini Makkah kuwahamisha Ahli zake na akawapa ngamia wawili na Dir-ham mia tano (500) ziwasaidie safarini.

(Wakarudi Madinah) na kumletea Fatma na Umuu kulthuum binti za Mtume wa Allah, na Bi. Saudah Bint Zum-ah mkewe (mtume).

Ama Bi Rukia (Bint mwingine wa Mtume) yeye alikwa amekwisha hama zamani pamoja na mumewe: Uthman Ibn Affaan.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *