NI MFUMO GANI KHASA WA MAISHA (DINI) ANAOUHITAJIA MWANADAMU?

Tumekuishaona kwamba dini ni mfumo Fulani wa maisha unaofuatwa na binadamu.

Sasa suala linalojitokeza ni je, ni mfumo upi wa maisha (dini) unaomfaa mwanadamu?

Tuanze kulijibu swali hili kwa kuanza kusema kwamba tangu zama za kale mwandamu amekuwa katika harakati za kupigania kupata maisha ya furaha na amani.

Si hivi tu bali pia kuunda jamii adilifu. Harakati hizi zinaaathiriwa kwa kiwango kikubwa na itikadi au mfumo maisha unaofuatwa na jamii husika.

Mfumo sahihi wa maisha au dini ya kweli inayomfaa mwanadamu na itakayokidhi kiu ya mwanadamu katika kupata maisha ya amani na furaha, ni lazima iwe:-

 

            1. Inalingana/inayokubaliana na maumbile ya mwanadamu na ulimwengu aishimo.

2. Na itikadi inayokubali kuhojiwa na kuingia akilini.

3. Inakidhi mahitaji asili ya kimaumbile ya mwanadamu kiroho na kimwili.

4. Inaweza kujibu maswali ya mwanadamu kuhusiana na uumbwaji huu wa ulimwengu  sambamba na yeye mwenyewe.

5. Inaweza kumuonyesha mwanadamu nafasi lengo na wajibu wake katika maisha haya.

6. Na uwezo wa kukidhi mahitaji ya kiakili, kimaono na kihaiba ya mwanadamu.

7. Ni dini ya ulimwengu mzima kwa ajili ya walimwengu wote kwa zama zote.

 

Kwa kuzingatia nukta hizi kama kigezo/mizania ya dini/mfumo sahihi wa maisha unaomfaa mwanadamu.

Tutaona kuwa hakuna mfumo unaoweza kuzigusa nukta zote hizi kwa ukamilifu zaidi ya ule Allah Mola Muumba aliowachagulia mwanadamu.

Na huu si mwingine bali ni mfumo Islamu.

One thought on “NI MFUMO GANI KHASA WA MAISHA (DINI) ANAOUHITAJIA MWANADAMU?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *