UONGO

Uongo au kusema uongo ni miongoni mwa tabia mbaya ambazo muumini wa kweli anapaswa kujiepusha nazo. Mwenyenyezi Mungu Mtukufu anatuambia:-

“WANAOZUA UWONGO NI WALE WASIOZIAMINI AYA ZA MWENYEZI MUNGU; NA HAO NDIO WAONGO” ?[16:105]

Kwa mujibu wa aya tabia ya kuzua uongo ni sifa waliyopambika nayo watu wasiyo waumini, muumini mkamilifu wa imani hawi muongo.

Mtume wa Mwenyezi Mungu aliulizwa: muumini anaweza kuwa mwoga? Akajibu “Ndiyo(anaweza)” Akaulizwa(tena): anaweza kuwa bakhili (Muumini)? Akajibu: “Ndiyo.” Akaulizwa (tena Muumini) anaweza kuwa muongo? Akajibu: Hapana Muumini hawi muongo.”

Ikiwa Bwana Mtume anaikanusha Imani kwa mtu mwenye tabia ya kusema uwongo, huo uwongo basi ni nini? Wanazuoni wanasema:

Uongo ni kueleza jambo au kitu kinyume na vile kilivyo kwa kujua au kutokujua, kwa makusudi au bila ya kukusudia. Bwana Mtume anasema:

“Atakayemwambia mtoto mdogo njoo uchukue (akaja) na asimpe (kitu) huo ni uongo.” Ahmad

Kwa nini mtu anasema uongo.? Nini sababu ya kusema uongo.?

Tabia hii ni mbaya inatokana na maumbile ya mwanadamu ya kutaka kujivutia manufaa na kujiondoshea madhara kwa hali na gharama yoyote ile.

Mwanadamu anaweza kuona kusema uongo ndiko kutakakomvua na kumuepusha na janga linalomkabili kama vile kufungwa jela au kufukuzwa kazi, hapo husema uwongo ili asalimike, pia hulazimika kusema uongo anapoona kusema ukweli kutamletea madhara kama vile kutoa ushahidi dhidi ya mzazi wake, ushahidi utakaopelekea ahukumiwe kifo, hapo husema uongo bila ya kujali kauli ya Bwana Mtume alipotuambia:

“Jilazimisheni (kusema) ukweli kwani ukweli humuongoza(mtu) katika wema na bila shaka wema humuongozea (mtu)katika uovu, na uovu (nao) humuongozea motoni na mtu huandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu muongo.” Bukhaariy na Muslim

Tabia hii mbaya ya kusema uongo ina madhara mengi sana kwa mzuaji uongo na kwa jamii kwa ujumla.

Muongo akibainika kwa kudhihiri ukweli, huaibika na kudharauliwa na jamii, pia hupoteza uaminifu kwa watu na akhera anangojewa na adhabu kali.

Mtu muongo pia husababisha chuki, uhasama na hata ugomvi baina ya watu.

Ni kutokana na madhara haya na mengineyo ndio sababu Uislamu umeikemea vikali tabia hii mbaya.

UONGO

Uongo au kusema uongo ni miongoni mwa tabia mbaya ambazo muumini wa kweli anapaswa kujiepusha nazo. Mwenyenyezi Mungu Mtukufu anatuambia:-

“WANAOZUA UWONGO NI WALE WASIOZIAMINI AYA ZA MWENYEZI MUNGU; NA HAO NDIO WAONGO” ?[16:105]

Kwa mujibu wa aya tabia ya kuzua uongo ni sifa waliyopambika nayo watu wasiyo waumini, muumini mkamilifu wa imani hawi muongo.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *