VITU VILIVYO NAJISI

Vitu vilivyo najisi ni pamoja na :

Mfu/Mzoga ila mwanadamu, samaki na nzige.

1. Kiungo cha mnyama kilichokatwa naye yu hai. Amesema Bwana Mtume :

“Kilichokatwa kwa nyama na ilhali yu hai hicho (kilichokatwa) ni mzoga” Abu Dawud.

2. Damu, mkojo, kinyesi (mavi) ya wanadamu, wanyama au ndege.

3. Nguruwe ! MwenyeziMungu anatuambia :

“SEMA SIONI KATIKA YALE NILIYOFUNULIWA MIMI KITU KILICHOHARIMISHWA KWA MLAJI KUKILA ISIPOKUWA KIWE NI MZOGA AU DAMU INAYOMWAGIKA AU NYAMA YA NGURUWE KWANI HIYO NI UCHAFU …” [6:145]

4. Mbwa kwa ushahidi wa hadithi isemayo

 “Mbwa atakaporamba chombo cha mmoja wenu basi na akimwage (kilichomo ndani) kishe akikoshe (chombo) mara saba”

5. Matapishi, usaha, maji ya madonda

6. Wadii na Madhii. Wadii ni maji mazito yatokayo baada ya mkojo kutokana na kazi ngumu/nzito. Madhii ni maji meupe yanayoteleza, haya hutoka wakati wa matamanio khafifu (kwa mfano kuchezeana baina ya mwanaume na mwanamke). Matamanio yakiwa ya nguvu ndio hutoka manii.

7. Tembo/Pombe kwa aina zake zote. MwenyeziMungu anasema :

“ENYI MLIOAMINI ! BILA SHAKA ULEVI NA KAMARI NA KUABUDIWA ASIYEKUWA ALLAH NA KUTAZAMIA KWA MSHARE YA KUPIGIA RAMLI (na kwa vinginevyo, yote haya) NI UCHAFU UTOKANAO NA KAZI YA SHETANI. BASI JIEPUSHENI NAVYO ILI MPATE KUFAULU” [5:90]

8. Maziwa ya mnyama asiyeliwa.

 

VITU VILIVYO NAJISI

Vitu vilivyo najisi ni pamoja na :

Mfu/Mzoga ila mwanadamu, samaki na nzige.

1. Kiungo cha mnyama kilichokatwa naye yu hai. Amesema Bwana Mtume :

“Kilichokatwa kwa nyama na ilhali yu hai hicho (kilichokatwa) ni mzoga” Abu Dawud.

2. Damu, mkojo, kinyesi (mavi) ya wanadamu, wanyama au ndege.

3. Nguruwe !

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *