KUPAKAZA MAJI JUU YA SOKSI

Naam, kunajuzu kupakaza maji juu ya soksi pale zitakapokuwa zimekamilisha soksi hizo masharti yote ya upakazaji juu ya khofu, kama yalivyoelezwa katika darasa zilizotangulia.

Sheykh Abdurahman Al-Jasiyriy – Allah amrehemu amesema katika kitabu chake kiitwacho “AL-FIQ-HU ALAL-MADHAAHIBIL – ARBAA.” Juzuuu ya I, ukurasa 113, chapa ya DAARUL-HADITH – Cairo ambayo mukhatasari wake ni kwamba wala hakuna tofauti baina ya kuwa khofu imetengenezwa kwa ngozi, au sufi nzito au pamba, na huitwa kilichotengenezwa kutokana na malighafi hizi (sufi/pamba) JAURABU (soksi) na jaurabu (maana yake) ni kile kivaliwacho mguuni kama ilivyo maarufu katika zama zetu hizi. Basi, hakika inaswihi kupakaza juu yake (jaurabu) wakati zitakapokuwa ni ngumu na imara. Haiswihi kupakaza juu ya soksi nyepesi ambazo haziwezi kuzuia maji kupitia ndani. ………..” Mwisho wa kunukuu.

Kisha akaendelea kusema tena: Kupakaza juu ya khofu kumethibiti kwa riwaya iliyopokelewa na Mughiyrah Ibn Shu’bah – Allah amuwiye radhi – “kwamba mtume – Rehema na Amani zimshukie – alipakaza juu ya soksi na makubadhi.”

2 thoughts on “KUPAKAZA MAJI JUU YA SOKSI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *