MTUME AFANYA IBADA KATIKA PANGO LA HIRAA

Mtume wa Mwenyezi Mungu – Rehema na Amani zimshukie – alipokaribia umri wa miaka arobaini alipenda kukaa peke yake faraghani na kujitenga na jamii yake; jamii ya watu wa Makkah.

Jamii iliyozama katika kiza cha ushirikina na tabia mbaya zisizo na chembe ya utu. Kujitenga huku hakukuwa ni kwa sababu alikuwa anaichukia jamii yake, la hasha. Bali ni kwa ajili ya kuyachukia maovu yaliyokuwa yakitendwa na jamii yake.

Kwa hivyo akaonelea ni vema akae faraghani atafakari ni jinsi gani atakavyoweza kuinusuru na kuitoa jamii yake katika itikadi ile potofu ya ushirikina, itikadi ya kuyaabudia masanamu yaliyotengenezwa na mikono yao wenyewe.

Baada ya kufikiri kwa kina, ni wapi katika mji wa Makkah ambapo anaweza kupata nafasi ya faragha, hakupapata.

Hapo ndipo akaamua atoke nje kabisa ya mji wa Makkah. Akaamua ajitenge kwa kukaa ndani ya pango la “Hiraa”.

Hiraa” ni pango dogo lililopo juu ya jabali Nuur. Jabali hili liko kiasi cha umbali wa wa maili tatu kutoka mji wa Makkah, mahala pasipo na nyumba wala mashamba.

Pango la “Hiraa” lilikuwa linatisha na lenye upweke mkubwa, upweke ambao ulizidishwa na kiza kilichotanda mahala pale.

Hapa ndipo Mtume aliona patamfaa kutafakari jinsi ya kuikomboa jamii yake kutokana na utumwa wa ushirikina.

Akawa anachukua chakula cha kutosha kutoka kwa mkewe Bi Khadija na kwenda zake faraghani katika pango la Hiraa.

Huko alikaa kiasi cha siku kumi na mara nyingi akitimiza mwezi kamili.

Kazi kubwa aliyokuwa akiifanya huko ilikuwa ni kumuabudu Mola wa haki kupitia mafundisho sahihi yaliyoachwa na babu yake, Nabii Ibrahim – Rehema na Amani ziwashukie wote -.

Athari ya mafundisho ya Nabii Ibrahim alikuwa ingali hai miongoni mwa makurayshi wachache ambao waliendelea kufanya ibada kwa mujibu wa mafundisho hayo.

Naye Mtume akawa anafanya ibada kwa kuufuata muongozo huo huo.

MTUME AFANYA IBADA KATIKA PANGO LA HIRAA

Mtume wa Mwenyezi Mungu – Rehema na Amani zimshukie – alipokaribia umri wa miaka arobaini alipenda kukaa peke yake faraghani na kujitenga na jamii yake; jamii ya watu wa Makkah.

Jamii iliyozama katika kiza cha ushirikina na tabia mbaya zisizo na chembe ya utu. Kujitenga huku hakukuwa ni kwa sababu alikuwa anaichukia jamii yake, la hasha. Bali ni kwa ajili ya kuyachukia maovu yaliyokuwa yakitendwa na jamii yake.

Kwa hivyo akaonelea ni vema akae faraghani atafakari ni jinsi gani atakavyoweza kuinusuru na kuitoa jamii yake katika itikadi ile potofu ya ushirikina, itikadi ya kuyaabudia masanamu yaliyotengenezwa na mikono yao wenyewe.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *