MTUME NA UCHUNGAJI KONDOO

Historia inatuambia kuwa kazi ya mwanzo kabisa iliyofanywa na Bwana Mtume ilikuwa ni uchungaji wa kondoo na mbuzi.

Aliamua kufanya kazi hii ile aweze kupata pesa za kujikimu mwenyewe na kumpunguzia Ami yake Abdul Mutwalib ukali wa maisha.

Hivyo Mtume – Rehma na Amani zimshukie – akaanza kuchunga kondoo na mbuzi wa watu wa Makkah kwa ujira mdogo aliokuwa akipewa.

Kituo cha kazi yake hii ilikuwa ni “Ajyaad”; hii ni jangwa lililokuwa nje kidogo ya mji wa Makkah, hapo ndipo alipokuwa akiwachunga wanyama hao.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ana hekima kubwa sana katika kuifanya shughuli hii ya uchungaji kuwa ndio kazi ya mitume.

Wanayaanza maisha yao kwa kuchunga wanyama na kuyahitimisha kwa kuwachunga binadamu wenziwao.

Amesimulia swahaba Jaabir bin Abdillah –Allah amuwie Radhi – akisema :

[Tulikuwa pamoja na Mtume – Rehma na Amani zimshukie – tukichuma matunda ya mabivu ya mpili mpili tawa, akasema

“Chumeni (matunda) yaliyo meusi kwani ndiyo matamu zaidi, mimi nilikuwa nikiyachuma wakati nilipokuwa ninachunga kondoo na mbuzi”. Tukamuuliza:

Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ulikuwa ukichunga kondoo na mbuzi ? Akajibu “Ndio na hakuna mtume yeyote ila alichunga”]

Kwa hiyo uchungaji wa kondoo ni alama nyingine inayothibitisha utume wa Nabii Muhammad. Mwenyezi Mungu amejaalia uchungaji wa wanyama kuwa ni chuo cha kutoa mafunzo ya uchungaji na uongozi kwa mitume wake.

 Wakiweza kuwachunga kondoo na mbuzi ambao hawa ni wanyama wanyonge zaidi kuliko wengine, nyoyo zao zitatawaliwa na huruma na upole.

Wakifuzu ma kuhitimu katika chuo hiki kinachotoa mafunzo ya uchungaji na uongozi, ndipo hupewa shahada zao kwa kukabidhiwa jukumu gumu na zito la kuwachunga binadamu wenziwao.

Kama walivoweza kuwastahamilia wanyama ndivyo wanavyotakiwa kuwavumilia wanadamu wenzao wenye tabia ngumu zilizosheheni ukukutavu wa moyo. Tunasoma ndani ya Qurani Tukufu juu ya ugumu wa nyoyo :

 “KISHA NYOYO ZENU ZIKAWA NGUMU BAADA YA HAYO (yote); HATA ZIKAWA KAMA MAWE AU NGUMU ZAIDI (kuliko mawe) … [2:74]

Ni watu kama hawa ndio ambao Bwana Mtume anapewa jukumu la kuwalea na kuwachunga.

 Kwa kuwa alihitimu vema chuoni, alifaulu kuifanya kazi yake hii ngumu kwa ufanisi mkubwa, ingawa ilimgharimu subira ya hali ya juu. Mwenyezi Mungu anamtunukia Mtume wake shahada ya kufaulu, pale aliposema :

 “BASI KWA SABABU YA REHEMA ITOKAYO KWA ALLAH UMEKUWA LAINI KWAO (Ewe Muhammad) NA KAMA UNGEKUWA MKALI NA MWENYE MOYO MGUMU BILA SHAKA WANGALIKUKIMBIA (usingelimpata hata mtu mmoja) ….” [3:159]

Hii ndiyo natija na matunda ya uchungaji wa wanyama na hiyo hekima yake kwa mukhtasari.

 

 

MTUME NA UCHUNGAJI KONDOO

Historia inatuambia kuwa kazi ya mwanzo kabisa iliyofanywa na Bwana Mtume ilikuwa ni uchungaji wa kondoo na mbuzi.

Aliamua kufanya kazi hii ile aweze kupata pesa za kujikimu mwenyewe na kumpunguzia Ami yake Abdul Mutwalib ukali wa maisha.

Hivyo Mtume – Rehma na Amani zimshukie – akaanza kuchunga kondoo na mbuzi wa watu wa Makkah kwa ujira mdogo aliokuwa akipewa.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *