SHARTI ZA KUSIHI UDHU

Sharti za kusihi udhu, haya ni mambo ambayo mwenye kutawadha ayahakikishe kwanza kabla hajaanza kutawadha, ili udhu wake uweze kusihi na kukubalika kisheria. Miongoni mwa sharti muhimu kabisa za udhu ni kama zifuatazo :

1. Kutokuwepo kizuizi kinachoweza kuyazuiliya maji wakati wa kutawadha kuufikilia ngozi, kwa sura ya maji kupita juu bila ya kufikilia ngozi. Kizuizi hiki chaweza kuwa ni mafuta mazito ya mgando, ute wa mshumaa, rangi ya lami, na vitu vyenye kufanana na hivi tulivyotaja.

2. Lisimpate mwenye kutawadha wakati wa kutawadha kwake jambo lenye kuubatilisha na kuutengua udhu wake, kama vile kutokwa na kitu katika mojawapo wa tupu mbili.

3.  Maji ya udhu yawe ni TWAHARA na yenye kufaa kutumika kwenye udhu.

4.  Kutakata mwanamke kutokana na damu ya hedhi na nifasi, kwani udhu hausihi wala kumpasa mwanamke aliye hedhini au nifasini mpaka atakapotahirika.

5. Uislamu wa mwenye kutawadha, kwani udhu si wajibu na wala hausihi kwa asiyekuwa muislamu, ajapofuata taratibu zote za udhu.

6. Kisiwepo juu ya kiungo cha udhu chochote kinachoweza kuharibu mojawapo ya sifa tatu za maji, ambazo ni tamu (ladha), rangi na harufu. Vitu hivi ni pamoja na vumbi la mkaa, chokaa, sementi na kadhalika.

SHARTI ZA KUSIHI UDHU

Sharti za kusihi udhu, haya ni mambo ambayo mwenye kutawadha ayahakikishe kwanza kabla hajaanza kutawadha, ili udhu wake uweze kusihi na kukubalika kisheria. Miongoni mwa sharti muhimu kabisa za udhu ni kama zifuatazo :

1. Kutokuwepo kizuizi kinachoweza kuyazuiliya maji wakati wa kutawadha kuufikilia ngozi, kwa sura ya maji kupita juu bila ya kufikilia ngozi. Kizuizi hiki chaweza kuwa ni mafuta mazito ya mgando, ute wa mshumaa, rangi ya lami, na vitu vyenye kufanana na hivi tulivyotaja.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *