TAMKO LA IQMA

Lifuatalo ndilo tamko kamili la iqaamah kama lilivyothibiti katika hadithi nyingi sahihi zilizopokelewa na maimamu Bukhaariy, Muslim na wengineo:

 

ALLAAHU AKBAR ALLAAHU AKBAR,

ASH-HADU AN LAA ILAAHA ILLAL-LAAH,

ASH-HADU ANNA MUHAMMADAN RASUULULLAAH,

HAYYA ALAS-SWALAAH, HAYYA ALAL-FALAAH,

QAD QAAMATIS-SWALAAH, QAD QAAMATIS-SWALAAH,

ALLAAHU AKBAR ALLAAHU AKBAR,

LAA ILAAHA ILLAL-LAAH.

 

Adhana hutolewa kwa sauti ya taratibu (kuvuta kidogo) wakati ambapo iqaamah hutolewa kwa sauti ya haraka kidogo.

Hii ni kwa sababu falsafa ya adhana ni kuwaita walio mbali, kwa hiyo njia ya utuvu wa sauti (Tartiyl) ikawa ndio ifikishayo zaidi wito.

 Na iqaamah inakusudia kuwainua watu waliohudhuria mahala pa swala kuswali, kwa hiyo ikawa kutolewa kwa sauti ya haraka haraka mithili ya mtu aamrishaye ndio kunanasibikiana zaidi na hali hii.

Hivi ndivyo Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie-alivyomwambia Bilali-Allah amuwiye radhi:

“Utapoadhini fanya utuvu (taratibu) na utapokimu fanya haraka”. Tirmidhiy

Mtu aliyepitwa na swala na akataka kuzikidhi (kuziswali nje ya wakati wake), ataadhini kwa ajili ya swala ya mwanzo tu na atakimu kwa kila swala.

Ushahidi wa hili ni kwamba Mtume-Rehema na Amani zimshukie:

“Alijumuisha Muzdalifah baina ya swala ya Maghribi na ile ya Ishaa kwa adhana moja na iqaamah mbili”. Muslim

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *