UTANGULIZI NASAHA

ZIJUE NASAHA ZA WIKI

Nasaha za wiki ni ukumbi wa kunasihiana, kubadilishana,kukosoana,kushauriana, na kuelimishana katika nyanja mbalimbali.

Tutakumbushana kupitia nasaha za wiki juu ya yale yatupasayo kutenda ama kutotenda kwa mujibu wa amri na maelekezo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Kadhalika nasaha za wiki itakuwa ikikuletea msimamo na kauli ya Uislamu juu ya kadhia/masuala mbalimbali yanayojitokeza ulimwenguni hivi leo kutokana na kupanuka na kukua kwa elimu ya sayansi na technolojia.

Masuala kama vile upandikizaji na viungo, watoto wa chupa., uzazi wa mpango, utoaji wa mimba na kadhalika.

 

CHIMBUKO NA MSINGI WA NASAHA ZA WIKI

Nasaha za wiki ni natija na zao la kauli tukufu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“NA WANAOAMINI WANAMUME NA WANAOAMINI WANAWAKE, NI MARAFIKI WAO KWA WAO . HUYAAMRISHA YALIYO MEMA NA HUYAKATAZA YALIYO MABAYA, NA HUSIMAMISHA SWALA NA HUTOA ZAKA NA HUMTII ALLAH NA MTUME WAKE. HAO NDIO AMBAO ALLAH ATAWAREHEMU. HAKIKA ALLAH NI MWENYE NGUVU NA MWENYE HEKIMA” [ 9:71]

Kadhalika nasaha za wiki zimejiegemeza katika kauli ya Bwana Mtume –Rehema na Amani za Allah zimshukie

“Yeyote miongoni mwenu atakayeuona uovu,basi auondoshe kwa mkono wake, kama hakuweza (kuuondosha kwa mkono) basi (auondoshe) kwa ulimi wake na kama hakuweza basi (achukie) kwa moyo wake na huko (kuchukia) ni imani dhaifu zaidi” Muslim.

Hizi ndizo hatua za kufuata katika kuuondosha uovu katika jamii kama alivyotuelekeza Bwana Mtume.

Uzoefu umethibitisha kuwa ugonjwa ukipuuzwa na kuachwa mwilini bila ya kupatiwa matibabu muafaka na katika wakati muafaka, maradhi hayo husambaa na kuenea mwilini na hatimaye husababisha madhara makubwa na pengine kifo.

Hali ni hiyo hiyo pia kwa maasi, uovu ukiachwa bila kukemewa na mtu akawa huru kutenda uovu bila kuulizwa wala kukatazwa, matokeo yake ni kufa kwa jamii kimaadili. Matokeo ni kuzaliwa jamii isiyo na chembe ya utu, jamii ya waenda uchi, jamii ya walevi, wavuta bangi na kadhalika.

Sasa ili kuepusha kujenga ukuta mzima kwa sababu ya kutokuziba ufa pale pale tu ujikokezapo.

Website yako WEBSITE UISLAMU ikaonelea ni vema ikakuletea fursa hii ya Nasaha za wiki ili uweze kujikumbusha na kujielimisha juu ya lipi utende upate radhi za Mola wako Muumba na lipi usitende ili uziepuke ghadhabu na adhabu kali za Mola wako aliye mkali mno wa kuadhibu. Mola wetu Mtukufu tunakuomba ututie chini ya kauli yako tukufu:

“……BASI WAPE HABARI NJEMA WAJA WANGU HAWA AMBAO HUSIKILIZA KAULI ( nyingi zinazosemwa), WAKAFUATA ZILE ZILIZO NJEMA, HAO NDIO ALIOWAONGOA ALLAH NA HAO NDIO WENYE AKILI” [39:17-18]

 

UTANGULIZI NASAHA

Nasaha za wiki ni ukumbi wa kunasihiana, kubadilishana,kukosoana,kushauriana, na kuelimishana katika nyanja mbalimbali.

Tutakumbushana kupitia nasaha za wiki juu ya yale yatupasayo kutenda ama kutotenda kwa mujibu wa amri na maelekezo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Kadhalika nasaha za wiki itakuwa ikikuletea msimamo na kauli ya Uislamu juu ya kadhia/masuala mbalimbali yanayojitokeza ulimwenguni hivi leo kutokana na kupanuka na kukua kwa elimu ya sayansi na technolojia.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *