KUANZA KWA ADHANA

Wakati wa swala ulipowadia alilingana mlinganiwa Mtume wa Allah – rehema na Amani zimshukie – akawaita watu kuja kuswali kwa kusema

Asswalaatu Jaamiah,” basi watu wakakusanyika kwa ajili ya swala. Kadhalika historia  imetusajilia kauli pinzani inayopingana na hii ya mwanzo.

Kauli hii iliyomo katika vitabu vya histora inasema watu walikuwa wanakusanyika kwa ajili ya swala bila ya wito wowote ule.

Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie  lilimshughulisha sana suala la adhana. Alifikiria ni jinsi gani ataratibu namna ya kuwajulisha watu kuwa wakati wa swala umeingia na hivyo wanawajibika kukusanyika kwa ajili ya kuitekeleza ibada ya swala.

Mtume akaitisha mkutano wa hadhara na kuwataka kushauri maswahaba katika suala hili. Maswahaba wakaitumia fursa hii vema kwa kuchangia fikra mbalimbali.

Baadhi ya maswahba wakashauri itumike kengele, igongwe kila unapoingia wakati wa swala kama wanavyofanya Manaswara.

Bwana Mtume hakuiafiki rai hii kwa sababu kufanya hivyo itakuwa ni kushabihiana na kuwaiga Manaswara.

Kundi jingine  likasema tupulize tarumbeta kama wafanyavyo Mayahudi, rai hii pia ikakataliwa na Mtume kwa hoja ile ile  ya kushabihiana na Mayahudi.

Maswahaba wakaendelea kuchangia fikra na mawazo na kusema tupige ngoma, mtu akisikia mlio wa ngoma hiyo atajua kuwa wakati wa swala umeingia Bwana Mtume hakuikubali rai hii kwa kuwa huo ulikuwa ni utaratibu uliokuwa ukitumiwa na warumi.

Wengine wakashauri uwashwe moto mkubwa utakaopanda juu angani na kuonekana na kila lmmoja kama wafanyavyo Majusi.

Mtume akaona si busara kutumia njia hii, kwa kigezo kuwa ni njia ya hatari na pia ni kuutukuza moto unaoabudiwa na Majusi.

Rai nyingine iliyotolewa ilikuwa ni  kusimikwa bendera mahala pa muinuko itakapoonekana na kila mtu, na hivyo kumfahamisha kila aionaye kuwa wakati wa swala umeingia.

Rai hii pia ilikumbana na upinzani wa wajumbe kwa hoja kuwa bendera itaonekana tu na yule  aliye nacho, aliyelala haitamsadia.

Kwa ujumla Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie hakukubaliana na fikra na rai zote hizi, kwa sababu zote zilikuwa tayari zinatumika na watu wa dini nyingine kuitana katika ibada zao potofu.

Mtume hakupenda  kushabiahiana na watu hawa wanaofuata dini (mifumo) potofu, alipenda Uislamu uwe na utaratibu wa pekee wa kuitana na kukusanyana kwa ajili ya swala.

Mkutano  huu wa hadhara ukamalizika bila ya kupatikana muafaka wowote juu ya suala la wito wa swala.

Wajumbe wakatawanyika kurudi majumbani mwao huku wakiamini kuwa bado wana jukumu la kutafakari mpaka waweze kupata utaratibu muafaka wa wote wa swala utakaoridhiwa na Mtume wa Allah Ibn Is-haaq – Allah amurehemu anasema:

“Baina ya wato kuwa katika hali hiyo (ya kutafakari), mara tahamaki hivi Abullah Ibn Zayd Ibn Tha’alabah – Al- answaariy akaona (akaota) usingizini wito wa swala. Akamuendea mbio Mtume wa Allah- Rehema na Amani zimshukie – Akamwambia,

“Ewe Mtume wa Allah, hakika imenitokea pepesi usiku wa leo. Amenipitia mtu mmoja aliyevaa nguo za kijani akiwa na kengele mkononi mwake, nikamwambia:

 Ewe mja wa Allah, unaniuza kengele hiyo? Akaniuliza: Unaitaka kwa ajili ya nini? Nikamjibu: Tuitumie kuwaita watu katika swala. Akaniambia: Je, nikufahamisha namna bora zaidi kuliko hiyo (unayotaka kuitumia)? Nikamuuliza: Ni ipi hiyo? Akaniambia sema:

 ALLAHU AKBAR ALLAHU AKBAR ALLAHU AKBAR ALLAHU AKBAR,

ASH-HADU AN LAAILAHA ILLA-LLAH, ASH-HADU AN LAAILAHA ILLA-LLAH,

ASH-HADU ANNA MUHAMMADAN RASULULULLAH, ASH-HADU ANNA MUHAMMADAN RASULULULLAH

HAYYA ALALSWALAAH, HAYYA ALALSWALAAH

HAYYAH ALALFALAAH,  HAYYAH ALALFALAAH

ALLAHU AKBAR ALLAHU AKBAR

LAA ILAHA ILLALLAH

 

Alipomueleza Mtume pepesi hiyo iliyomtokea, Mtume – Rehema na Amani zimshukie – akasema,

“Hakika bila ya shaka hiyo ni ndoto ya haki (kweli) pindipo atakapo Allah, inuka pamoja na Bilali ukamfundisha aadhini kwa kutumia maneno hayo kwani yeye ndiye mwenye sauti kali yenye kwenda mbali zaidi kuliko wewe.

Bilali aliyotoa adhana kama alivyofundishwa kwa amri ya Mtume, Sayyidna Umar Ibn Khatwaab akaisikia adhana hiyo akiwa nyumbani kwake.

Akatoka kumuendea Mtume wa Allah huku akipita na kuburura nguo yake kutokana na haraka aliyokuwa nayo, akamwambia Mtume:

Ewe Mtume wa Allah, ninamuapia yule ambaye aliyekupeleka kwa haki nimeona usingizini mithili ya maneno haya aliyoyaona! Mtume wa Allah – Rehema na Amani zimshukie akasema: “Himda zote njema zinamstahikia Allah kwa hilo

 

Hii ndio adhana na hivyo ndivyo ilivyoanza katika mwaka wa kwanza wa Hijrah. Ibn Saad – Allah amrehemu – anasema: Wito wa ASSWALATU JAAMIA uliokuwa ikitumika kabla ya adhana hii iliyoidhinishwa na kupitishwa na Bwana Mtume uliendelea kutumiwa.

Ulitumika katika hali ya dharura kila ilipojitokeza kama vile vita.

Waislamu waliitwa kwa wito huu, wakakusanyika kuja kusikiliza kulikoni hata.

Kama si wakati wa swala. Kumbukumbu sahihi za kihistoria zinaonyesha kwamba kulikuwa na waadhini wawili katika mji wa Madinah zama za uhai wa Bwana Mtume. Muadhini mkuu akiwa ni Sayyidna Bilali na msaidizi wake alikuwa ni Abdullah Ibn Umuu Maktum.

Bilali alikuwa akisema kaitka adhana ya Sub-hi baada ya HAYYA ALALFALAAH maneno haya ASSALAATU KHAYRUN MINANNAWM.

 Bwana Mtume akamsikia akiyasema maneno hayo, akayakubali na hivyo yakaendelea kutumika hadi hii leo.

Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie aliamrisha paadhiniwe adhana mbili katika alfajiri ya mwezi wa Ramadhani. Adhana ya kwanza ililenga kuwaamsha waliolala kwa ajili ya kula daku, ama ile ya pili ndio ilikuwa adhana kwa ajili ya swala.  

KUANZA KWA ADHANA

Wakati wa swala ulipowadia alilingana mlinganiwa Mtume wa Allah – rehema na Amani zimshukie – akawaita watu kuja kuswali kwa kusema

Asswalaatu Jaamiah,” basi watu wakakusanyika kwa ajili ya swala. Kadhalika historia  imetusajilia kauli pinzani inayopingana na hii ya mwanzo.

Kauli hii iliyomo katika vitabu vya histora inasema watu walikuwa wanakusanyika kwa ajili ya swala bila ya wito wowote ule.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *