VIKOSI VYA UJASUSI VYATUMWA KUCHUNGUZA NYENDO ZA MAADUI

Wanasira na wanatarekh (wanazuoni wa fani za Sira naTarekh) wana istilahi (terminologies) wanazozitumia wanapoandika habari zihusianazo na vikosi vya vita vya Mtume.

 Hutumia neno “sariyah” kumaanisha kikosi cha vita ambacho mtume hakuwemo. Na kile kikosi alichoshiriki Mtume hukiita “ghaz-wah”, hata kama hayakutokea mapambano.

Vita/mapambano hayakuwa ndio lengo la vikosi hivi, hili linathibitika kutokana na idadi ndogo iliyounda vikosi hivi.

Idadi hii ndogo haikutosha kuvipa vikosi hivi uwezo wa kuanzisha mapambano. Kwa hivyo basi itakudhihirikia kuwa lengo khasa la kutumwa vikosi hivi, ilikuwa ni kuchunguza nyendo na harakati za adui.

Wakati mwingine yakitokea mapambano mepesi yaliyohusisha urushianaji wa mishale, pale vikosi hivi vinapokutana na adui ana kwa ana.

Waumini waliyatumia mapambano hayo kumtia khofu adui yao na kumfanya awe na hisia kwamba waislamu wana nguvu na uwezo wa kukabiliana nae.

Tafiti zilizofanywa na wanasira na wanatarekh zinaonyesha kuwa kimsingi lengo la kuundwa na kutumwa kwa vikosi hivi lilikuwa:-

Kuunda nguvu za kijeshi zitakazokuwa zikizunguka baina ya Madinah na Makkah. Kwa lengo la kuhakikisha kuwa mji wa Madinah hauvamiwi na kushambuliwa ghafla.

Kuwakaribia Makurayshi kwa mashambulizi mepesi ya ghafla yatakayokata mawasiliano baina ya Makkah na Shamu.

Kukatika kwa mawasiliano baina ya pande mbili hizi hakutamaanisha kingine zaidi ya kudhoofika nguvu za Makurayshi za kiuchumi na kijeshi.

Vikosi hivi viliwafanya Makurayshi kuwa katika hali ya tahadhari kila mara na hivyo kuwaondoshea hali ya utulivu na amani.

Ikawa sasa wanatumia gharama maradufu katika kuhakikisha usalama wa misafara yao ya kibiashara.

Kwa kuchelea kuwa isije kuangukia mikononi mwa waislamu na kuwaongezea nguvu. Kwa ujumla utumaji wa vikosi hivi ulikuwa na msaada mkubwa sana kwa upande wa waislamu.

 Vikosi hivi vilichangia kwa kiasi kikubwa kuwatia khofu maadui na kuwafanya wafikirie mara mbili mbili kabla ya kuamua kuchukua hatua yo yote dhidi ya waislamu.

Kwa upande mwingine viliwasaidia waislamu kujua nyendo na mikakati ya baadae ya maadui. Mapatano ya kusaidiana (league) baina ya waislamu na makabila ya Kiarabu.

Yaliyokuwa yakiishi katika jangwa lililo baina ya Makkah na Madinah, ni moja ya matunda ya vikosi hivi.

Viongozi wa makabila haya walichukua dhima na ahadi ya kushirikiana na waislamu pindipo watakaposhambuliwa. Na kwamba makabila haya hayatajiunga na Makurayshi au adui mwingine wa waislamu na kuwa pamoja nae dhidi ya waislamu.

MAKURAYSHI WAJARIBU KUTUMIA FURSA YA KOSA LILILOFANYWA NA WAISLAMU.

Cheche zilizowasha moto mkali baina ya pande mbili hizi;waislamu na makurayshi, ni ile “sariyah” ya Abdullah Ibn Jahshi.

Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie-alimtuma Abdullah kuongoza kundi la Muhajirina wasiopungua wanane, wakapeleleze khabari za Makurayshi.

Mtume akamuandikia barua na akamuamrisha asiifungue ila baada ya kwenda mwendo wa siku mbili.

Akishaifungua na kuisoma baada ya siku mbili hizo, atekeleze maagizo yaliyomo na wala asimlazimishe ye yote katika watu aliopewa kuwaongoza.

Abdullah alipokwenda nao mwendo wa siku mbili, akaifungua ile barua aliyopewa na Mtume, tahamaki akakuta imeandikwa:

“Utakapoisoma barua yangu hii, endelea kwenda mpaka ufike mahala paitwapo {Nakhlah} baina ya Makkah na Twaif. Hapo wangojelee Makurayshi na utuletee khabara zao”. Akasema baada ya kusoma:

“Usikivu na utii”, na akawaambia wale wenzake yale yaliyoandikwa ndani ya barua ile ya Mtume.

 Na akazidi kuwaambia Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-amenikataza kumlazimisha ye yote miongoni mwenu.

Basi anayetaka kufa shahidi pamoja nami na anifuate na asiyetaka na ashike njia arudi. Ama mimi ninasonga mbele kuitekeleza amri ya Mtume wa Allah.

Akasonga mbele na wakasonga pamoja nae wote aliokuwa nao, hakuna hata mmoja aliyerejea nyuma.

Isipokuwa mabwana Sa’ad Ibn Abiy Waqaasw na Utbah Ibn Ghaz-waan ndio walibakia nyuma kwa ajili ya kumtafuta ngamia wao aliyepotea, ambaye walikuwa wakimpanda kwa zamu.

Abdullah na wenzake wengine wakaendelea na safari mpaka wakafika “Nakhlah”, kama walivyoamrishwa na Bwana Mtume.

Hapo wakasadifu kukutana na msafara wa Makurayshi ukija kutokea pande za Twaif, ukiwa na shehena ya zabibu, ngozi na bidhaa nyingine.

Msafara huu ulikuwa unaongozwa na watu wanne tu, ambao ni; Abdullah Ibn Al-hadhwramiy, Uthman Ibn Al-Mughiyrah na Naufal na Al-Hakam Ibn Al-Kaisaan.

Kukutana kwa makundi mawili haya kulikuwa ni katika siku ya mwisho ya mwezi wa Rajab. Abdullah akashauriana na wenzake wachukue hatua gani kuhusiana na msafara ule wa Makurayshi. Wakaambizana baada ya mashauriano mafupi:

Wallah! Lau mkiwaacha waende zao usiku huu wa leo, wataingia Haram (Makkah) na wataitumia mali hii dhidi yenu.

Na mkipigana nao mtakuwa mmepigana katika mwezi mtukufu, ambao ni haramu kupigana. Wakasita na wakaogopa kuwasogelea, wakiwa katika hali hiyo ya kusita na kutaka kuwasogelea, ndipo wakashajiishana na kutiana mori.

Wakauvamia msafara ule na kuushambulia, katika purukushani hizo wakamuua Abdullah Ibn Al-Hadhwramiy; mmoja wa walinzi wa msafara ule.

Na kuwateka wengine wawili na mmoja akafanikiwa kukimbia. Bwana Abdulah na wenzake wakarejea Madinah na ngawira yao ile ya msafara na mateka wawili.

Walipofika kwa Mtume na kumuhadithia mambo yalivyokuwa, Mtume alighadhibika na kusema: “Mimi sikuwaamrisha kupigana katika mwezi mtukufu”.

Akakataa kupokea ngawira ile, Abdullah na wenzake wakahemewa wasijue la kufanya.

Wakajutia kitendo chao kile na wakayakinisha kuwa wameangamia na waislamu wenzao wakawa wanawalaumu kutokana na kitendo walichokifanya.

Makurayshi kwa upande wao wakakichukulia kitendo kile cha Abdullah na wenzake kuwa ni fursa muafaka ya kuwachochea waarabu kupigana na Mtume.

Wakaanza kueneza khabari miongoni mwa waarabu kwamba Muhammad na maswahaba wake wamevunja utukufu na heshima ya mwezi mtukufu.

Khabari za tukio hili ziliwafadhaisha sana watu mpaka wakafikia kujiuliza kwa mshangao:

Hivi vita hupiganwa katika mwezi mtukufu, tena iwe hivyo kwa Muhammad ambaye yeye ndiye anadai kumtii Allah na anailingania dini ya haki?!

Waislamu Madinah waliposikia tuhuma hizo nzito dhidi ya wenzao na dini yao khasa, walianza kuchukua hatua za kujibu shutuma hizo na kuwatetea wenzao.

 

Wakisema kuwa yote yaliyofanyika hayakufanyika ndani ya mwezi mtukufu wa Rajab, bali yamefanyika ndani ya mwezi wa Shaabani.

 Kwa kweli tukio hili liliwafurahisha mno maadui wa Uislamu. Mayahudi nao hawakubakia nyuma katika kulifurahia hili.

Kutokana na tukio hili, wao waliamini kuwa sasa ni lazima vita itokee baina ya waislamu na makurayshi, bali na waarabu wote.

Kwa sababu ya kuvunjwa heshima/utukufu wa mwezi mtukufu na waislamu. Kisha wao kama kunguru wakae pembeni wakitazama ugomvi wa panzi.

Kwa ujumla hali ya hewa ya kisiasa ilichafuka sana baina ya waislamu kwa upande mmoja na makurayshi na pamoja na makabila mengine ya kiarabu kwa upande mwingine. Na yakasemwa mengi kuhusiana na kadhia hii.

 

VIKOSI VYA UJASUSI VYATUMWA KUCHUNGUZA NYENDO ZA MAADUI

Wanasira na wanatarekh (wanazuoni wa fani za Sira naTarekh) wana istilahi (terminologies) wanazozitumia wanapoandika habari zihusianazo na vikosi vya vita vya Mtume.

 Hutumia neno “sariyah” kumaanisha kikosi cha vita ambacho mtume hakuwemo. Na kile kikosi alichoshiriki Mtume hukiita “ghaz-wah”, hata kama hayakutokea mapambano.

Vita/mapambano hayakuwa ndio lengo la vikosi hivi, hili linathibitika kutokana na idadi ndogo iliyounda vikosi hivi.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *