MWENENDO NA SILKA YA MTUME KABLA YA KUPEWA UTUME

Bwana Mtume –Rehma na Amani zimshukie- alijulikana miongoni mwa jamii yake kwa sifa na tabia zake njema kama vile ukweli, uaminifu, haya, unyenyekevu na upole.

Jamii yake ilimkubali na ikampa jina la MKWELI MUAMINIFU. Huu ulikuwa ndio umaarufu wake pale mjini Makkah na kwingineko.

Jamaa zake na jamii nzima walimuheshimu na kumpenda kwa kuwa alikuwa ni mtu mwepesi kuzoeleka na alishirikiana katika kazi mbali mbali za maendeleo katika jamii yao.

Kutokana na tabia njema hizi alizopambika nazo Bwana Mtume, watu walikuwa wakienda kuweka amana zao kwake.

Waliamini kuwa nyumbani kwa Mtume ndio mahala salama pa kuweka amana zao ambapo wanaweza kuzipata wakati wowote wakizihitajia hata kama ni usiku.

Lakini pamoja na mapenzi na heshima aliyoivuna Mtume kutoka kwa jamii yake, ikiwa ni jazaa ya tuzo na tabia zake njema kwao bado alihisi dhiki ndani ya nafsi yake.

Bwana Mtume hakuichukia jamii yake kama watu bali alikerwa na tabia zao mbaya na itikadi yao potofu ya ushirikina.

Hili ndilo lililomsumbua na ili kuonyesha chuki yake dhidi ya tabia na itikadi potofu ya jamii yake, hakupata kushirikiana nao katika kunywa pombe hata mara moja kiasi cha kuwashangaza walio wengi kwani ulevi lilikuwa ni jambo la kawaida kwa jamii ile mbali ya kuwa ni fakhri.

 Kadhalika hakuhudhuria hata mara moja sherehe na ibada za miungu sanamu japokuwa jamii yake ilimsihi sana ashirikiane nao lakini alikataa.

Haya yote hayakuwa ila ni kwa fadhila zake Mwenyezi Mungu ambaye ndiye aliyemuhifadhi Mtume wake kutokana na uchafu ule wa kijahili.

Kwa mukhtasari hivyo ndivyo Mtume alivyoishi na jamii yake kabla hajakabidhiwa rasmi dhamana ya Utume.

MWENENDO NA SILKA YA MTUME KABLA YA KUPEWA UTUME

Bwana Mtume –Rehma na Amani zimshukie- alijulikana miongoni mwa jamii yake kwa sifa na tabia zake njema kama vile ukweli, uaminifu, haya, unyenyekevu na upole.

Jamii yake ilimkubali na ikampa jina la MKWELI MUAMINIFU. Huu ulikuwa ndio umaarufu wake pale mjini Makkah na kwingineko.

Jamaa zake na jamii nzima walimuheshimu na kumpenda kwa kuwa alikuwa ni mtu mwepesi kuzoeleka na alishirikiana katika kazi mbali mbali za maendeleo katika jamii yao.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *