SIRA NI NINI?
Sira ni fani inayojishughulisha kuelezea maisha ya Nabii Muhammad tangu kuzaliwa mpaka kufa kwake, ikiwa ni pamoja na malezi na makuzi yake, wasifu wake wa kimaumbile, tabia zake, harakati zake katika kuufikisha ujumbe wa Uislamu kwa ummah, mahusiano yake na watu na mataifa mbalimbali.
Pia sira inaelezea hali ya ulimwengu kijamii na kiitikadi kabla na baada ya kuja Nabii Muhammad, kadhalika inataja maisha na utawala wa Makhalifa waongofu baada ya Mtume.
MADHUMUNI NA FAIDA ZA SIRA
Fani ya Sira inalenga kumfahamisha Muislamu:-
- Taswira na mfumo mzima wa Uislamu unatolewa na kutafsiriwa na maisha ya Mtume.
- Maisha ya Nabii Muhammad ndio kigezo na mfano mwema wa kuigwa na kufuatwa ili kuweza kupata mafanikio Duniani na Akhera. Mwenyezi Mungu atuambia:-
“BILA SHAKA MNAO MFANO MWEMA KWA MTUME WA MWENYEZI MUNGU…”(33:21)
- Muislamu apate katika maisha ya Nabii Muhammad kitu kitakachomsaidia kuifahamu Qur-ani kwani aya nyingi za Qur-ani zinafasiriwa na kuwekwa wazi na matukio yaliyotokea katika uhai wa Mtume.
- Sira inaonyesha ni njia na mbinu zipi alizozitumia Mtume mpaka akaweza kuusimamisha Uislamu katika ulimwengu uliokuwa umefunikwa na kiza totoro cha ushirikina.
- Sira inaonyesha ni jinsi gani Mtume alivyoyatatua matatizo na vikwazo mbalimbali vya ndani na nje alivyokumbana navyo katika kumfikisha ujumbe wa Allah kwa watu wote.
Hizi ni baadhi tu ya faida zinazopatikana katika kuisoma na kuifuata sira ya Bwana Mtume.
Mashaaallah