HUKUMU NA DALILI YA KUTAYAMAMU

Kutayamamu ni WAJIBU/FARDHI kwa mtu katika hali mbili:

1: Wakati atakapoyakosa maji ya kutawadhia.

2: Wakati atakaposhindwa kuyatumia maji kwa sababu zilizobainishwa na sheria.

 

Kutayamamu kumethibiti katika Qur-ani Tukufu, Sunnah na Ijmaa. Dalili ya kutayamamu katika Qur-ani ni kauli tukufu ya Mwenyezi Mungu:

“………… NA MKIWA WAGONJWA AU MMO SAFARINI, AU MMOJA WENU AMETOKA CHOONI AU MMEINGILIANA NA WANAWAKE NA HAMKUPATA MAJI, BASI KUSUDIENI (tayamamuni) UDONGO (mchanga) ULIO SAFI (twahara) NA KUUPAKA NYUSO ZENU NA MIKONO YENU …” [5:6].

Tayamamu katika Suna imo katika kauli ya Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie – aliposema :

“….na tumejaaliwa (tumefanyiwa) ardhi yote kuwa ni msikiti (mahala pa kuswalia) na mchanga (udongo) wake umefanywa kwetu ni twahara (utwahirishayo) tutakapokuwa hatukupata maji”. Muslim.

Ama Ijmaa, wanazuoni wote wamekogomana na kukubaliana kuwa tayamamu imefanywa kuwa ni sheria, itumike badala ya ya udhu na josho katika hali na mazingira maalum yaliyobainishwa na sheria.

Hiyo ndiyo tayamamu ndani ya Qur-ani, Sunnah na Ijmaa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *