SHARTI ZA KUWAJIBISHA SWALA YA IJUMAA (WANAOWAJIBIKIWA NA IJUMAA)

Swala ya Ijumaa kwa mujibu wa sheria ni wajibu kwa mtu ambaye zimepatikana kwake sharti saba zifuatazo:-

Uislamu: Swala ya Ijumaa ni wajibu kwa muislamu tu na wala haimuwajibikii kafiri kwa kuwa hana sifa ya Ijumaa, ambayo ni Uislamu.

Baleghe: Swala ya Ijumaa inamuwajibikia mtu mzima aliyefikia umri wa baleghe. Kwa maana hiyo, swala ya Ijumaa si wajibu kwa mtoto mdogo; aliye chini ya umri wa baleghe.

Akili timamu: Inamuwajibikia swala ya Ijumaa mtu mzima mwenye akili timamu. Kwa hivyo basi, mwendawazimu hawajibikiwi na swala hii ya Ijumaa.

Uhuru kamili (Uungwana): Swala ya Ijumaa si wajibu kwa mtumwa anayezingatiwa na sheria. Hii ni kwa sababu ya kushughulishwa kwake na haki ya utumwa kwa bwana wake. Haki hii ya bwana wake ndio inayomnyima uwajibu wa swala ya Ijumaa.

Uanamume: Ijumaa si wajibu kwa wanawake wa Kiislamu kwa sababu ya kushughulika kwao na ulezi wa watoto na shughuli za nyumbani. Pia Ijumaa si wajibu kwao kutokana na imkani (uwezekano) ya kupatikana mashaka kwao kwa sababu ya ule uwajibifu wa kuhudhuria katika wakati na mahala maalum.

Siha (afya) ya kiwiliwili: Swala ya Ijumaa si wajibu kwa mgonjwa ambaye anapata maumivu (machungu) kutokana na harakati za kuhudhuria msikitini au kukaa msikitini mpaka kumalizika kwa swala.

Pia anapewa hukumu ya mgonjwa mtu ambaye anamuuguza na kumtumikia mgonjwa na pakawa hapana mtu wa kumshikia zamu wakati wa kwenda msikitini.

Huyu bila ya kuangalia mgonjwa ni ndugu au si ndugu yake wa nasabu, haimuwajibikii swala ya Ijumaa maadam mgonjwa anahitajia huduma yake.

Ukazi wa mahala pa Ijumaa: Ijumaa si wajibu kwa msafiri aliyesafiri safari ya halali ijapokuwa ni ile inayohusisha rukhsa ya kukusuru. Hukumu hii ni iwapo safari yake ilianza kabla ya kuchomoza kwa alfajiri ya siku ya Ijumaa.

Sharti saba hizi za uwajibifu wa swala ya Ijumaa ambazo ni: Uislamu, baleghe, akili timamu, uungwana, uanamume, siha ya mwili na ukaazi wa mji. Zote hizi zinatokana na kauli hizi za Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie:-

ü      “Ijumaa ni haki ya wajibu juu ya kila muislamu katika/pamoja na jamaa ila watu wanne:

·        mtumwa aliyemilikiwa, au

·        mwanamke, au

·        mtoto mdogo, au

·        mgonjwa”. Abuu Daawoud-Allah amrehemu.

ü      “Ye yote mwenye kumuamini Allah na siku ya mwisho (muislamu), basi imemuwajibikia Ijumaa ila mwanamke, msafiri, mtumwa na mgonjwa”. Daaruqutwniy na wengineo-Allah awarehemu.

SHARTI ZA KUWAJIBISHA SWALA YA IJUMAA (WANAOWAJIBIKIWA NA IJUMAA)

Swala ya Ijumaa kwa mujibu wa sheria ni wajibu kwa mtu ambaye zimepatikana kwake sharti saba zifuatazo:-

Uislamu: Swala ya Ijumaa ni wajibu kwa muislamu tu na wala haimuwajibikii kafiri kwa kuwa hana sifa ya Ijumaa, ambayo ni Uislamu.

Baleghe: Swala ya Ijumaa inamuwajibikia mtu mzima aliyefikia umri wa baleghe. Kwa maana hiyo, swala ya Ijumaa si wajibu kwa mtoto mdogo; aliye chini ya umri wa baleghe.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *